Rais Samia afanya uteuzi, mabadiliko wizara mbili

February 6, 2026 9:54 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Uapisho wa viongozi hao utafanyika katika tarehe itakayopangwa.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi, uhamisho wa viongozi mbalimbali Serikalini pamoja na mabadiliko ya muundo katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Nishati.

Taarifa ya Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu iliyotolewa usiku wa leo Februari 6, 2026 inabainisha kuwa mabadiliko hayo yaliyofanywa katika wizara hizo yatafanya idadi ya makatibu wakuu katika wizara hizo kuwa wawili kwa kila wizara.

“Dk Tausi Mbaga Kida ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji,” imesema taarifa ya Machumu iliyorejea taarifa ya Katibu Mkuu Moses Kusiluka.

Wengine walioteuliwa kujaza nafasi hizo mbili katika Wizara ya Nishati ni Dk James Peter Mataragio ambaye atashughulikia masuala ya mafuta na gesi asilia na Mhandisi Felchesmi Jossen Mramba atashughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.

Kabla ya uteuzi huo Dk Mataragio alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, nafasi aliyoitumikia kwa miaka miwili tangu Februari, 2024.

Rais Samia pia amemteua Balozi Waziri Rajab Salum kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Dk Hashil Twaib Abdallah ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Katiika hatua nyingine kiongozi huyo wa nchi amefanya uteuzi wa naibu katibu mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Balozi, mwenyekiti wa bodi, wakuu wamikoa wawili, makatibu tawala wa mikoa wawili na naibu makatibu wakuu nane.

Aidha, uapisho wa viongozi hao utafanyika katika tarehe itakayopangwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
29 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
29 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
29 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fidia yakwamisha wakazi 27 Kigogo kuhama mabondeni, ‘El Nino’ ikikaribia

Fidia yakwamisha wakazi 27 Kigogo kuhama mabondeni, ‘El Nino’ ikikaribia

Nukta TV

Haya ndio maeneo ghali zaidi kuishi Dar es Salaam

Haya ndio maeneo ghali zaidi kuishi Dar es Salaam

Nukta TV

Fahamu athari za matumizi ya feni, kiyoyozi kiafya.

Fahamu athari za matumizi ya feni, kiyoyozi kiafya.

Nukta TV