Rais Samia afanya uteuzi Muhimbili, BoT, TMA,TEITI

January 29, 2026 6:11 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kati yao yupo Dk Ladislaus Benedict Chan’ga aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu TMA.

Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wanne katika taasisi mbalimbali nchini.

Taarifa ya Bakari Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu iliyonukuu taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka iliyotolewa leo Januari 29, 2026 inabainisha kuwa walioteuliwa ni pamoja na Dk Rahma Salim Mahfoudh.

“Dk Mahfoudh ameteuliwa kuwa Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akichukua nafasi ya Julian Banzi Raphael ambaye amemaliza muda wake,” imesema taarifa ya Machumu.

Mwingine ni Dk Ladislaus Benedict Chan’ga aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) baada ya kaimu nafasi hiyo kwa kipindi kirefu.

Prof. Muhammad Bakari Kambi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akichukua nafasi ya Dkt. Ellen Mkondya Senkoro ambaye amemaliza muda wake.

Pamoja na hao Rais Samia pia amemteua Balozi Wilson Kajumula Masilingi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania (TEITI) akichukua nafasi ya CPA. Ludovick Utouh ambaye amemaliza muda wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks