Rais mstaafu Benjamin Mkapa afariki dunia, Tanzania ikitangaza siku saba za maombolezo

July 24, 2020 4:05 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 81. 
  • Rais John Magufuli ametangaza kifo hicho usiku wa kuamkia leo Ijumaa Julai 24, 2020.
  • Pai ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Ijumaa Julai 24, 2020. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Ijumaa Julai 24, 2020 kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa wamu ya tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea Jijini Dar es Salaam.

Rais John Magufuli ametangaza kifo hicho usiku wa kuamkia leo kupitia televisheni ya Taifa (TBC) kuwa marehemu Mkapa amefariki dunia katika hospitali moja jijini humo. 

”Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe Watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. 

“Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki,” amesema Rais Magufuli.

                     

Aidha, Rais John Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Ijumaa Julai 24, 2020 kufuatia kifo cha Rais mstaafu Mkapa huku akiwataka Watanzania kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 

“Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti,” imeeleza taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kueleza kuwa taarifa zingine kuhusu msiba huo wa kitaifa zitatolewa baadaye.

Rais Magufuli amesema amesikitishwa na kifo cha rais Mkapa na Taifa limempoteza mtu imara aliyekuwa na mapenzi na nchi yake.

Mkapa alikuwa Rais wa Tanzania kati ya mwaka 1995 na 2005 kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Alizaliwa Novemba 12, 1938.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV