Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia

February 29, 2024 5:32 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bendera kupepea kwa nusu mlingoti kwa siku saba.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia leo Februari 29 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Mwinyi aliyekuwa Rais wa Tanzania kati ya mwaka 1985 hadi 1995 alikuwa  akiugua ugonjwa wa Saratani ya mapafu tangu mwezi Novemba mwaka 2023.

Matibabu yake yalianzia nchini London na baadae alihamishiwa katika hospitali ya Mzena alipouguzwa ambako mauti yamemkuta.

Aidha, Rais Samia ametangaza maombolezo ya kitaifa kwa siku saba  huku bendera ikipepea nusu mlingoti.

“Kwa niaba ya Serikali natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu wa kitaifa,” amesema Rais Samia katika hotuba yake fupi aliyoitoa usiku wa Februari 29, 2024.


Soma zaidi:Air Tanzania yasema ndege ilipata ‘hitilafu ya kawaida’


Historia ya maisha ya mwinyi

Mwinyi alizaliwa Mei 8, 1925 katika kijiji cha Kivule, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Safari yake ya elimu ilianza mwaka 1933 akiwa na miaka nane ambapo alipelekwa katika Shule ya msingi Manga Pwani iliyopo Zanzibar aliposoma hadi darasa la nne na baadae kuendelea na darasa la tano katika shule ya Dole alikohitimu darasa la nane mwaka 1942.

Aliendelea na masomo ya Diploma katika Chuo Kikuu cha Dublin Uingereza kati ya mwaka 1954 hadi 1956.

Kiongozi huyo pia anacheti cha umahiri wa lugha ya kiingereza, alichohitimu katika taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na cheti cha umahiri wa lugha ya kiarabu alichohitimu, Cairo, Misri, mwaka 1972 hadi 1974.74.

Kuhusu siasa Mwinyi alianza kwa kulijiunga na chama cha Afro Shiraz (ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbali mbali za serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile katibu mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya,

Nyadhifa nyingine alizoshika kiongozi huyo ni Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri na ilipofika waka 1985 alichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya pili  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hayati Rais Mwinyi atakumbukwa kwa mageuzi ya sera ambapo aliruhusu sera za kiliberali zilizochochea pakubwa ukuaji wa sekta binafsi na kukuza kasi ya maendeleo nchini Tanzania hata kupachikwa jina maarufu la “Mzee Ruksa”

Endelea kutufuatia kufahamu zaidi kuhusu historia ya mwinyi na ratiba za mazishi

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV