Prof. Mkenda azindua ujenzi wa shule ya wasichana Simanjiro
Dar es Salaam. Serikali imepiga hatua nyingine katika kuimarisha elimu ya wasichana baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tukuta, iliyopo Kata ya Terat, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Mradi huo unatekelezwa na Shirika la ECLAT Development Foundation Tanzania kwa ufadhili wa Upendo Foundation kutoka Ujerumani, ukiwa na thamani ya zaidi ya Sh4.6 bilioni.
Kati ya kiasi hicho, Sh216 milioni zinahusiana na thamani ya ardhi iliyotolewa na kijiji.
Hata hivyo, maswali yanabaki, je, juhudi hizi za ujenzi wa shule mpya zinatosha kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa elimu kwa wasichana, hasa katika maeneo ya vijijini kama Simanjiro?
Kwa mujibu wa kitabu cha hali ya uchumi mwaka 2024,idadi ya shule za sekondari iliongezeka na kufikia 6,269 mwaka 2024 kutoka shule 5,926 mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 5.8.ย

Kwa upande wake Profesa Mkenda amesisitiza kuwa Serikali bado inahitaji ushirikiano zaidi na wadau ili kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Elimu. Picha l Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Kati ya hizo, shule 4,905 zilikuwa za Serikali na shule 1,364 zisizo za Serikali.
Ongezeko la idadi ya shule lilitokana na jitihada za Serikali za kuongeza idadi ya madarasa na shule mpya za sekondari pamoja na uwekezaji wa sekta binafsi.ย
Aidha, mwaka 2024, idadi ya wanafunzi katika shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita ilikuwaย milioni 3.3ย ikilinganishwa na wanafunzi milioni 3.0 mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 7.7 ambapo kati ya hao, wasichana walikuwa 1,753,013.
Kwa upande wake Profesa Mkenda amesisitiza kuwa Serikali bado inahitaji ushirikiano zaidi na wadau ili kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Elimu.ย
Ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2027 kila mtoto atalazimika kusoma hadi kidato cha nne, hatua inayopanua elimu ya lazima kuwa miaka 10.ย
Mkurugenzi wa Upendo Foundation, Dkt. Fred Heimbach, amepongeza jitihada za Serikali katika sekta ya elimu na kuhimiza jamii kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya msingi ya elimu.ย
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Terat, Bw. Kone Medukenya, amesema shule hiyo itakuwa na vyumba vya madarasa 12, maabara za sayansi 4, mabweni 6, nyumba za walimu 16, jengo la utawala, chumba cha kompyuta na seva, bwalo la chakula, jiko, ukumbi, kisima kirefu cha maji na uzio wa shule.ย
Latest