Nukta Africa, Unesco yawanoa waandishi mbinu za uthibitishaji wa habari

October 17, 2022 6:58 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mwendelezo wa mafunzo kuwafikia wanahabari na wahariri 100 nchi nzima ifikapo Disemba 2022.
  • Wanahabari wasisitizwa kuyazingatia mafunzo ili yawasaidie kutatua changamoto mbalimbali.

Dar es Salaam. Awamu ya tatu ya mafunzo kwa waandishi wa habari na wahariri nchini Tanzania yanayotolewa na kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa  yanaendelea leo kwa washiriki kufundishwa kuhusu uthibitishaji wa habari (fact checking).

Awamu mbili za mafunzo haya yanayofadhiliwa na Shirika la kimataifa la  Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ziliangazia uandishi wa habari za takwimu pamoja na mbinu za kutumia dijitali katika kuzalisha maudhui (multimedia storytelling) yenye msaada kwa jamii.

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa njia ya mtandao yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 17 hadi 19,2022.


Zinazohusiana:


Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa Nuzulack Dausen amewaambia wanahabari na wahariri kuyazingatia mafunzo hayo ili waweze kudhibiti ueneaji wa habari za uzushi unaokua kwa kasi.

“Ni matumaini yangu mtatumia vema mafunzo haya, mtajifunza namna gani mnaweza kutumia dijitali kuthibitisha taarifa au kuandika taarifa kwa usahihi zaidi. Mafunzo haya yatakuwa msaada pia kwa waandishi wa habari za uchunguzi,” amesema Dausen.

Jumla ya waandishi wa habari na wahariri 100 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo haya ya miezi mitatu mara baada ya awamu zote tatu kukamilika.

Mafunzo hayo ni moja ya mipango ya UNESCO chini ya Programu ya Kimataifa ya Maendeleo katika Mawasiliano (International Programme for the Development of Communication) yenye lengo la kuwezesha wanahabari na vyombo vya habari katika nchi zinazoendelea kuwa na uwezo wa kujitegemea na kuandika habari zenye mchango mkubwa kwenye jamii.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW