Nukta Afrika, Unesco wazindua mafunzo maalum kwa wanahabari

September 26, 2022 10:01 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni siku tatu za mafunzo ya ‘multimedia storytelling’.
  • Mafunzo hayo  yanalenga kuwawezesha waandishi kutumia vizuri mbinu za teknolojia kuzalisha maudhui yenye mchango mkubwa kwenye jamii.

Dar es Salaam. Kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu (Unesco) wamezindua mafunzo maalum ya siku tatu kuwajengea uwezo waaandishi wa habari kuandika kwa usahihi habari zao. 

Mafunzo hayo yanayoanza leo Septemba 26 hadi 28, 2022 yanahusu ‘multimedia storytelling’ ambayo yanalenga kuwawezesha waandishi kutumia vizuri mbinu za teknolojia kuzalisha maudhui yenye mchango mkubwa kwenye jamii.

Wanahabari tumieni fursa kuboresha taaluma

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UNESCO Dar es salaam, Nancy Angulo amesema ni vyema waandishi wa habari na wahariri kuzingatia mafunzo hayo ili waweze kuboresha taaluma zao.

“Naamini mafunzo haya yatawasaidia waandishi wa habari kudevelop (kuboresha) taaluma zao,” amesema Angulo.

Mafunzo ya ‘multimedia storytelling’ ni moja ya mipango ya UNESCO chini ya Programu ya Kimataifa ya Maendeleo katika Mawasiliano (International Programme for the Development of Communication) yenye lengo la kuwezesha wanahabari na vyombo vya habari katika nchi zinazoendelea kuwa na uwezo wa kujitegemea.


Soma zaidi


Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen ameishukuru UNESCO kwa kuona umuhimu wa  kufadhili mafunzo hayo kwa wanahabari na wahariri nchini ili kuboresha taaluma zao. 

Pia amewasisitiza waandishi wa habari na wahariri kuzingatia mafunzo yanayotolewa na kuyafanyia kazi  ili kupata matokeo chanya kwenye kazi zao watakazozalisha mara baada ya mafunzo hayo.

“Tunaamini mkitoka hapa mtaenda kufanyia kazi haya mafunzo ambayo mmeyapata hapa,” amesema Dausen.

Mafunzo hayo ni sehemu ya programu ya miezi mitatu yanayotolewa kwa awamu tatu kwa wanahabari na wahariri 100 ambao watajifunza kuhusu uthibitishaji habari, uandishi wa habari za takwimu na ‘multimedia storytelling’.

Kupitia mafunzo hayo waandishi wa habari na wahariri watapata nafasi ya kujifunza mbinu mpya za kuandaa habari zenye viwango  zinazoendana na mahitaji ya kitafaifa na kimataifa. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW