Nukta Africa kuongoza mijadala ya AI, uandishi wa habari za takwimu Arusha

April 27, 2026 5:09 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa lengo la kuimarisha uelewa na matumizi ya teknolojia za kisasa katika tasnia ya habari, pamoja na kukuza uwezo wa uandishi wa habari za takwimu na uthibitishaji wa taarifa.

Dar es Salaam. Kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa inatarajia kuongoza mjadala kuhusu akili unde (AI) na uandishi wa habari za takwimu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika kitaifa kuanzia Aprili 28 hadi 30, 2026 jijini Arusha ni miongoni mwa majukwaa makubwa yanayokutanisha wadau wa sekta ya habari na mawasiliano nchini kwa lengo la kujadili maendeleo, changamoto na fursa zilizopo katika tasnia hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Nuzulack Dausen amesema mijadala hiyo itakayofanyika katika maadhimisho hayo inalenga kuimarisha uelewa na matumizi ya teknolojia za kisasa katika tasnia ya habari, pamoja na kukuza uwezo wa uandishi wa habari za takwimu na uthibitishaji wa taarifa.

“Tutashiriki uzoefu wetu lakini mbinu ambazo zinaweza zikafanya anga la habari kuwa salama na lenye taarifa zenye ubora wa hali ya juu;” amesema Dausen.

Kwa takribani miaka nane, Nukta Africa imekuwa mdau muhimu katika sekta ya habari na mawasiliano nchini Tanzania kupitia utoaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari yanayoendana na mahitaji ya soko la sasa, ikiwemo kozi za uthibitishaji  habari (Fact-Checking), uandishi wa habari za takwimu (Data Journalism), ubunifu wa infografia (Infographics Design), na usimamizi wa maudhui ya kidijitali (Digital Content Management).

Kwa mujibu wa Dausen, uandishi wa habari za takwimu umekuwa ukikua taratibu nchini si kwa sababu hadhira haipendi aina hiyo ya habari, bali kutokana na changamoto ya ujuzi wa jinsi ya kuziwasilisha kwa namna inayoeleweka.

“Ndio maana Nukta Africa tumekuwa tukitoa mafunzo kuwapa uwezo waandishi wa habari na wapenda habari kuelewa, kuchambua na kuwasilisha taarifa za takwimu kwa njia rahisi na inayoeleweka,” amesema Dausen.

Wadau mbalimbali kushiriki

Mbali na Nukta Africa wadau wengine ambao pia ni sehemu ya waandaaji wa maadhimisho hayo ni Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Jamii Africa ambao wataongoza mijadala mingine kuhusu sekta ya habari na mawasiliano ili kuendelea kukuza uelewa wa pamoja.

Mbali na kushiriki katika mijadala hiyo, Nukta Africa pia inatarajia kuzindua Nukta AI, programu ya akili unde iliyobuniwa kurahisisha upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi zenye muktadha wa Tanzania, ili kuwasaidia watumiaji wa taarifa hususan vijana kufanya maamuzi bora ya kiuchumi na kijamii.

Aidha, Dausen ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta ya habari, teknolojia na mawasiliano kushiriki katika maadhimisho hayo ili kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuchangia mawazo yatakayosaidia kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
1 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
1 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Matarajio ya wachambuzi wa siasa na uchumi kwa Ndejembi

Nukta TV

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Maagizo mazito ya Rais Samia kwa Ndejembi

Nukta TV

Ndejembi alivyoapa mbele ya Rais Samia kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Ndejembi alivyoapa mbele ya Rais Samia kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Nukta TV