Njia zitakazosaidia biashara kupata faida kubwa, kudumu muda mrefu

February 22, 2019 6:25 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Jifunze kuweka rekodi ya matumizi yako na kuwa na menejimenti nzuri itakusaidia kuongeza nguvu ya kufanya vizuri katika kampuni yako.
  • Anza kupanga mikakati ya nani ataendeleza kampuni hata usipokuwepo ili iweze kudumu kwa muda mrefu zaidi.
  • kuwa na uwezo wa kukabili matumizi yako ili uweze kujua njia nzuri ya kutunza fedha.

Dar es Salaam. Kila mjasiriamali au mfanyabiashara ndoto yake kubwa ni kuona kampuni yake inakua na kudumu kwa muda mrefu.

Mbali na kukua, kampuni inatakiwa ilete faida mwaka hadi mwaka ambayo itaiwezesha kujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha zaidi mfukoni za mwekezaji au mwanzilishi wake. 

Safari ya kuifanya kampuni ijiendeshe yenyewe na kuzalisha faida siyo ya kitoto. Ni safari ya machozi na damu. 

Baadhi ya wazoefu na waliofanikiwa katika uendeshaji wa biashara wamekuwa wakitoa mbinu ambazo zitasaidia biashara changa kukua na hatimaye kuanza kutengeneza faida.

Katika wasilisho maalum kwa wajasiriamali Februari 21, 2019, Ofisa Mkuu wa Fedha toka benki ya biashara ya UBA, Chomete Hussein alitoa mbinu muhimu kwa wajasiriamali hao jinsi ya kuendesha kampuni au biashara ili iweze kuleta faida


Jifunze kuweka rekodi

Hussein amewashauri wajasiriamali hao kuwa na tabia ya kurekodi vitu mbalimbali wanavyofanya ili waweze kujua mwenendo wa biashara zao na wapi wanakwama na kwa kiasi gani wanaweza kujisahihisha ili waweze kusonga mbele. Kila taarifa ya mapato na matumizi iwekwe kwenye kumbukumbu vizuri.

“Unatakiwa upange vitu vizuri, kuwa na mfumo wa benki na tunza kumbukumbu zako inaweza hata kushawishi watu kuwekeza,” amesema Hussein.

Wajasiriamali wa kampuini changa wakimsikiliza kwa ukaribu na Chomete Hussein akiwapa mbinu za kufanya kampuni zao kukua katika mkutano uliowakutanisha Seedspace jijini Dar es Salaam. Picha| Zahara Tunda.

Kuwa na menejimenti nzuri 

Hapa anasema kuwa ni lazima kampuni iwe na menejimenti nzuri na yenye watu wanaojua taaluma zao ili kuleta ufanisi katika kazi.
Anasema kuwa unaweza kuwa na mawazo mazuri ya kibiashara lakini ukawa hauna uwezo wa kuendesha vizuri hivyo ni vyema ukawaajiri watu wanaoweza kuifanya na wewe ukabaki kuwa msimamizi ili mwisho wa siku uweze kukua kibiashara.

Kuwa na uwezo wa kukabili matumizi

Hussein anashauri wajasiriamali wawe na uwezo wa kukabili matumizi katika uendeshaji wa biashara zao. Unatakiwa ujue matumizi yako yapoje na ulitumia wapi kwa misingi gani na unawezaje kuirudisha pesa hiyo.

“Usipoweka kumbukumbu utaishia kusema chuma ulete,” amesema Hussein.

Vilevile kwenye biashara, anasema hata kama ulitoa pesa kwa mambo binafsi inapaswa iandikiwe na kuwe na namna ya kupima mahesabu.


Zinazohusiana: Unayafahamu majukumu aliyonayo mwekezaji kwenye ‘startups’?

                          Utambulisho, uwekezaji kuzibeba ‘Startups’ Tanzania


Tabia ya baadhi ya wajasiriamali kutumia fedha kwa matumizi bila kurejesha fedha hizo baadaye si rafiki na inaua biashara haraka.

Kwa uzoefu, Hussein anasema mwanzo wa biashara pesa huwa inayotumika zaidi kuliko iliyotoka lakini kama ukiendelea kuwa na matumizi mengi bila faida inapaswa uanze kufikiria unakosea wapi.

Wafanyabiashara wanaochipukia kwenye kampuni changa hawana budi kusaka maarifa zaidi ili waweze kufikia malengo yao.Picha| Zahara Tunda.

Kuwa na mbinu za kukabidhisha kampuni kwa wengine ili iweze kuendelea zaidi

Hapa mtaalam huyo anawashauri wajasiriamali wenye kampuni changa kuwa na mipango endelevu juu ya kampuni zao kwa sababu wengi wanakufa na kampuni kutokana na kutokuwa na mazoea ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya kukabidhi kwa wengine.

Mfano, anasema benki ya UBA imeweza kukaa miaka zaidi ya 70 kwa sababu wapo watu wanaoindeleza alipoishia mwanzilishi.

“Kama mjasiriamali uwe na uwezo wa kumpa mtu mwingine mawazo ili yaweze kudumu,” amesema Hussein.

Hata hivyo, anaeleza wazi kuwa yote hayo yatawezekana kama tangu siku ya kwanza utaweza kutambua mshahara wako ni upi na unawezaje kuwa na mzunguko wa pesa utakaoweza kuleta maslahi katika kampuni yako.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV