Nishati safi ya kupikia, kitendawili kigumu Tanzania

February 23, 2024 2:45 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asilimia 67 wanatumia kuni na asilimia 25 wanatumia mkaa kupikia.
  • Asilimia 88 ya kaya za vijijini zinatumia nishati zisizo salama kupikia
  • Wadau wa nishati waeleza suluhu ya kumaliza matumizi ya kuni, mkaa nchini.

Dar es Salaam. Licha ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, bado zaidi ya nusu ya kaya nchini hutumia kuni katika shughuli za mapishi, jambo linalotajwa kuathiri afya na mazingira.

Ripoti ya Utafii wa Athari za Upatikanaji wa Nishati Endelevu kwa mwaka 2021/2022 inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inabainisha kuwa asilimia 67 ya kaya zote Tanzania Bara hutumia kuni kama chanzo kikuu cha nishati kwa ajili ya kupikia.

Hiyo ni sawa na kusema zaidi ya nusu au kaya sita kati ya10 zinatumia nishati hiyo kwa ajili ya mapishi huku asilimia 25 wakitumia majiko ya mkaa na asilimia 8.1 majiko mengine.


Zinazohusiana: Nishati safi ya kupikia kunusuru maisha ya watu 33,000 kila mwaka Tanzania


Kwa mujibu wa takwimu hizo,Tanzania bado ina safari ndefu kufikia malengo endelevu (SDG) ya kuondoa matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ikiwemo mkaa na kuni.

Ili kufikia malengo ya hayo ya kidunia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa (UN) Serikali ilizindua Dira ya Taifa ya kuhamia katika nishati safi ya kupikia ili kuiwezesha Tanzania kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ifikapo mwaka 2030.

Jiko la mawe lilobuniwa na Mtanzania Raymond James ni miongoni wa majiko yanayotumia nishati mbadala inayosaidia kupunguza ukataji miti nchini.Picha |Daudi Mbapani/Nukta Africa.

Ngoma nzito vijijini

Licha ya malengo hayo, ripoti ya NBS inaweka wazi kuwa asilimia 88 ya kaya zilizopo vijijini zinatumia kuni kama chanzo kikuu cha mapishi, kulinganisha na asilimia 6 ya kaya zinazotumia nishati hiyo mjini.

Idadi hiyo ni sawa na kusema kaya nane kati 10 zilizopo vijijini bado zinazotumia nishati ya kuni kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia. 

Wakati huo huo, asilimia mbili tu ya wakazi wa vijijini ndio wanaotumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi.


Soma zaidi:Tamaduni zinavyodumaza vipaji wa wasichana mkoani Mwanza


Matumizi hayo ya majiko ya gesi katika maeneo ya vijijini yako chini mara 17 zaidi ya maeneo ya mijini kama Dar es Salaam ambapo asilimia 34 ya kaya zinayatumia nishati hiyo.

Kwa baadhi ya mikoa kama Simiyu, Singida, na Geita kaya tisa kati ya 10 zinatumia nishati ya kuni kupikia, huku matumizi ya nishati safi ya kupikia yakiwa chini ya asilimia 17 jambo linalohatarisha mazingira na afya za watumiaji.

Aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba Oktoba, 2022, aliwaambia wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa matumizi  ya kuni na mkaa kupikia husababisha watu 33,000 kupoteza maisha.

Hiyo inatokana na sumu zilizopo kwenye moshi unaotoka katika nishati hizo ambazo huathiri afya ya mtumiaji.

Mbali na takwimu hizo, Shirika la Afya Duniani (WHO) linabainisha kuwa takriban watu milioni 3.2  hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuvuta hewa chafu inayozalishwa na nishati za kupikia majumbani.

Hewa hizo husababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa ya mapafu, na ya mfumo wa hewa.Wadau wa nishati wasema tafiti ndio suluhu

Mtaalamu wa kujitegemea wa masuala ya nishati Thabiti Mikidadi, ameiambia Nukta habari kuwa ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa nchini Serikali inapaswa kufanya utafiti kufahamu mikakati inayopaswa kutumika kulingana na maeneo.

“Kila wilaya ipewe kazi ya kutafuta njia ya kuhakikisha watu wnahama katika matumizi ya kuni na mkaa kwa kufanya utafiti, kushuka chini kwa wananchi kuangalia mnyororo wa thamani ukoje,” amesema Mikidadi.

Pia ametoa rai kwa wadau wa nishati na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO) kuongeza nguvu katika mapambano hayo ili kunusuru mazingira maisha ya wananchi yanayopotea kutokana na athari za matumizi ya kuni na mkaa.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV