Nini kitatokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu ?

September 11, 2026 4:32 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuna makundi manne tu ya watu wenye kinga kisheria zinazowapa hiari ya kuitikia au kutokuitikia wito wa Mahakama wa kwenda kutoa ushahidi.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imekubali ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, la kuwaita Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camilius Wambura, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili. 

Uamuzi huo umetolewa jana, Septemba 10, 2026, chini ya Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, baada ya Lissu kuiomba Mahakama hiyo kutoa wito kwa mashahidi 7 aliowataja, akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Dk Philip Mpango, aliyekuwa Makamu wa Rais, Kassim Majaliwa, aliyekuwa Waziri Mkuu, pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa. 

Hata hivyo, Mahakama imekataa ombi la kuwaita viongozi hao wanne, ikisema kuwa ushahidi wao haukuwa muhimu kwa utetezi, na kusisitiza kuwa Jamhuri ndiyo yenye wajibu wa kuthibitisha mashtaka, si mshtakiwa kuthibitisha kutokuwa na hatia.

Kwa sasa, kinachosubiriwa ni kutolewa kwa wito wa Mahakama kwa mashahidi hao watatu waliokubaliwa ili wafike na kutoa ushahidi wa kumtetea Lissu, ambaye amekuwa mahabusu kwa zaidi ya siku 500.

Hivyo, swali linabaki, je mashahidi hao wataitikia wito wa Mahakama? 

Je, Sheria inasemaje nini iwapo mtu atakaidi kuitikia wito huo?

Wakili William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) amesema kuna makundi manne tu ya watu wenye kinga kisheria zinazowapa hiari ya kuitikia au kutokuitikia wito wa Mahakama wa kwenda kutoa ushahidi.

Hata hivyo katika makundi hayo hakuna Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) wala Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), hivyo viongozi hao hawana kinga hiyo inayowapa hiari ya kukataa kuitikia wito wa Mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Nukta TV

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Nukta TV

Jinsi waajiri wanavyokimbilia 'Interns' kukwepa ajira za kudumu

Jinsi waajiri wanavyokimbilia 'Interns' kukwepa ajira za kudumu

Nukta TV