Mahitaji teknolojia saidizi kwa walemavu yazidi kuongezeka duniani

May 17, 2022 9:59 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Takriban watu bilioni moja kati yao wanakosa fursa ya ufikiaji wa vifaa hivyo. 
  • Watu bilioni 2.5 wanahitaji kifaa kimoja au zaidi cha usaidizi.

Dar es Salaam. Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Dunia (WHO) na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF) imefichua kuwa zaidi ya watu bilioni 2.5 wanahitaji kifaa kimoja au zaidi cha usaidizi ikiwemo viti mwendo, vifaa vya usaidizi wa  kusikia au programu zinazosaidia mawasiliano na utambuzi.

Mkurugenzi wa WHO, Dk Tedros Ghebreyesus akizungumza Mei 16, 2022 Geneva, Uswisi amesema vifaa hivyo vya teknolojia ya usaidizi ni muhimu sana kwa kuwa vinabadili maisha na kufungua milango ya elimu kwa watoto wenye ulemavu.

Vifaa hivyo vinasaidia watu kupata ajira na kuimarisha mwingiliano wa kijamii kwa watu wazima wanaoishi na ulemavu, na pia vinasaidia wazee kuwa na  maisha huru na ya utu. 

 Wakati takwimu zinaonesha kuwa watu bilioni 2.5 wanauhitaji , takriban watu bilioni moja kati yao wanakosa fursa ya ufikiaji wa vifaa hivyo na wengi wao wanatoka katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Uchambuzi wa nchi 35 iliofanywa na ripoti hiyo ya teknolojia ya usaidizi unaonesha pengo kubwa kati ya nchi tajiri na zinazoendelea ambapo wakati ufikiaji ukiwa asilimia 3 katika mataifa maskini na ya kipato cha kati, kwenye mataifa tajiri uwezekano wa wananchi kupata vifaa hivyo vya usaidizi ni asilimia 90.

“Kuwanyima watu kupata zana hizi za kubadilisha maisha siyo tu ni ukiukaji wa haki za binadamu, bali ni jambo la kutoona mbali kiuchumi. Tunatoa wito kwa nchi zote kufadhili na kuweka kipaumbele kwa upatikanaji wa teknolojia ya usaidizi na kutoa nafasi kwa  kila mtu kuishi kulingana na uwezo wake,” amesema Dk Tedros.


Soma zaidi;


Mapendekezo yaliyotolewa na ripoti hiyo

Ripoti imeainisha  kuwa kadri idadi ya watu inavyoendelea kuongezeka duniani na watu wenye uhitaji wa vifaa vya usaidizi huenda kuongezeka hadi kufikia watu bilioni 3.5 ifikapo mwaka 2050.

Serikali zimeshauriwa kuhakikisha wenye uhitaji wanafikiwa na vifaa hivyo na mapendekezo 10 madhubuti ya kuweza kufikia hatua hiyo ni:

1. Kuboresha ufikiaji wa ndani wa  mifumo ya elimu, afya na huduma za kijamii.

2. Hakikisha kuna upatikanaji, usalama, ufanisi na uwezo wa kumudu wa vifaa vya usaidizi.

3. Kuongeza, kupanua na kuboresha uwezo wa wafanyakazi.

4. Kuwashirikisha kikamilifu watumiaji wa teknolojia za usaidizi na familia zao.

5. Kuongeza ufahamu wa umma na kupambana na unyanyapaa.

6. Kuwekeza katika takwimu na sera zinazozingatia kuwepo kwa ushahidi.

7. Kuwekeza katika utafiti, uvumbuzi, na mifumo ikolojia wezeshi.

8. Kuendeleza na kuwekeza katika mazingira wezeshi.

9. kujumuisha teknolojia ya usaidizi katika utatuzi wa masuala mengine ya uhitaji wa kibinadamu.

10.Kutoa usaidizi wa kiufundi na kiuchumi kupitia ushirikiano wa kimataifa ili kusaidia juhudi za kitaifa.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW