Ndege ya Tanzania iliyokamatwa Canada yaachiliwa, kutua Mwanza

December 12, 2019 7:20 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais Magufuli athibitisha kuwa imeachilia na itarejea nchini hivi karibuni. 
  • Ndege hiyo itakapowasili nchini itapokelewa katika uwanja wa ndege jijini Mwanza. 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada imeachiwa na wananchi watatangaziwa siku ya kuwasili ili waipokee jijini Mwanza.

Rais Magufuli aliyekuwa akizungumza na wajumbe wa Halmasharuri kuu ya Taifa ya chama cha Mapinduzi leo (Desemba 12, 2019) jijini Mwanza siku ya ndege hiyo kurudi na kupokelewa itatangazwa hapo baadaye.

Hata hivyo, amesema ndege hiyo itakapowasili nchini itapokelewa katika uwanja wa ndege jijini Mwanza. 

“Kwa taarifa tu ndege yetu iliyokuwa imeshikwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokelea hapa Mwanza,” amesema Rais


Soma zaidi:


Mamlaka nchini Canada zilikamata ndege hiyo, kutokana na shauri la kesi iliyofunguliwa na mkulima mstaafu raia wa Namibia, Hermanus Steyn.

Steyn pia alifungua kesi nchini Afrika Kusini mwezi Agust iliyosababisha ndege aina ya Air Bus 220-300 izuiliwe na hatimaye serikali ya Tanzania kushinda kesi mahakamani

“Mhe. Rais ndege yetu aina ya Bombadier ambayo ilipaswa ifike Tanzania kutokea Canada imekamatwa na mtu yule yule ambaye aliikamata ndege yetu kule Afrika ya Kusini.” alisema Prof. Kabudi,  Novemba 23 jijini Dodoma katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Msemaji Geita: Vijana msikurupuke kuja Katoro

Nukta TV

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV