Nchi 18 zisizosheherekea sikukuu ya Krismasi
- Ni nchi ambazo zina misimamo mikali ya kidini na kitamaduni.
- Katika baadhi ya nchi hizo, ni kosa kisheria kusheherekea Krismasi
- Zingine zimeruhusu baadhi ya matukio ya sikukuu hiyo.
Sherehe za Krismasi hufanyika kwa njia tofauti, huku nchi mbalimbali kote ulimwenguni zikiadhimisha msimu wa sikukuu hiyo kwa mila na desturi zao.
Mataifa machache yasiyo ya Kikristo hayatambui Krismasi na hayana aina yoyote ya sherehe za kitaifa, mapumziko au maadhimisho ya kuashiria kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Takribani nchi 40 hazina mapumziko rasmi za kitaifa wakati wa Krismasi, ingawa zaidi ya nusu ya mataifa hayo huwa na angalau aina fulani ya maonyesho ya kitaifa, kama vile mti wa Krismasi.
Kwa mujibu wa chombo cha habari za The Week cha nchini Uingereza, hizi ndizo nchi 18 zilizosalia ambazo watu wake hawasherehekei Krismasi kwa njia yoyote:
Afghanistan
Taifa hilo lenye Waislamu wengi limekuwa na uhusiano wenye misukosuko na Ukristo na sikukuu zake kwa miongo kadhaa. Hii iliongezeka wakati wa utawala wa Taliban wa miaka ya 1990, na hakuna dalili kuwa kundi hilo limebadili msimamo wake kuhusu Krismasi.
Mvutano kati ya Wakristo na imani nyingine za walio wachache nchini Afghanistan huenda ukaendelea hivi sasa baada ya kundi hilo la itikadi kali kutawala tena nchi hiyo. Krismasi haisherehekewi nchini humo na wale wanaojaribu kufanya hivyo hukabiliwa na vitisho.
Algeria
Taifa jingine lenye Waislamu wengi, Algeria halijawahi kusherehekea Krismasi katika sherehe zozote rasmi za kitaifa tangu lilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa, ambalo ni taifa lenye Wakatoliki wengi, mwaka 1962.
Hata hivyo, baadhi ya wahamiaji wa Kikristo wa Kiafrika nchini humo, pamoja na wanadiplomasia na wenyeji hufanya sherehe hiyo.
Bhutan
Ikiwa na idadi ya Wakristo wapatao 10,000 tu ( sawa chini ya 1% ya jumla ya raia wote), Krismasi si sehemu ya kalenda ya Bhutan kabisa, ambapo dini ya Ubuddha huchukua nafasi ya kwanza.
Brunei
Sherehe za hadhara za Krismasi zimepigwa marufuku katika jimbo dogo la Kiislamu la Brunei lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu 2015, huku mtu yeyote atakayepatikana akikiuka sheria hiyo akikabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela au faini ya Dola za Marekani 20,000 (Sh46 milioni) au vyote kwa pamoja.
Ingawa wasio Waislamu wanaruhusiwa kusherehekea sikukuu hiyo ndani ya jumuiya zao, na hawaruhusiwi kushiriki mipango yao na Waislamu wa nchi hiyo, ambao ni takriban theluthi mbili ya wakazi.
Kwa mujibu wa Wizara ya Masuala ya Kidini ya nchi hiyo, sheria hizo “zinalenga kudhibiti kitendo cha kusherehekea Krismasi kupita kiasi na kwa uwazi, jambo ambalo linaweza kuharibu aqidah (imani) ya umma wa Kiislamu”.
Mtaalamu mmoja aliiambia UCANew.co.uk kuwa “njia pekee ya kufurahia msimu wa sherehe ni kutoka kwa ya ajili likizo”.

China
Kulingana na gazeti la Daily Express, Krismasi nchini China ni “siku kama siku zingine za kazi na shule, ofisi na maduka hufunguliwa”, na kuongeza: “Nchi hiyo sio ya kidini, kwa hivyo Krismasi ilipigwa marufuku kabisa.”
Mnamo mwaka wa 2018, viongozi walianza “kushughulika na kupinga Krismasi”, na raia waliamriwa kutokusherehekea “badala yake kuzingatia kukuza utamaduni wa jadi wa Wachina”, liliandika gazetu la The Guardian.
Comoro
Ikiwa na asilimia 98 ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, visiwa vya Comoro katika Bahari ya Hindi vina msimamo thabiti dhidi ya Ukristo.
Uislamu wa Sunni umekuwa ni dini ya Serikali kufuatia kura ya maoni ya mwaka 2018, ambayo taasisi ya World Watch Monitor iliripoti “ilitarajiwa kuwa na athari kali kwa Wakristo wachache nchini humo.”
WorldAtlas iliripoti kwamba matukio ya wazi ya Kikristo yamepigwa marufuku, na Comoro “imekuwa kwenye orodha ya WorldWatch kwa miaka 22 iliyopita kwa kutesa Wakristo.”
Libya
Hakuna likizo za mwisho wa mwaka katika taifa hili lenye Waislamu wengi kwa miaka mingi.
Hata hivyo, kila tarehe 24 Desemba huwa ni siku ya uhuru wa nchi, ambayo inatoa sababu ya kusherehekea.
Mauritania
Licha ya kuwa na idadi ndogo ya Wakristo ndani ya mipaka yake, Serikali ya Mauritania imeamua kutowatambua kabisa, huku sensa ya hivi karibuni ikidai kuwa asilimia 100 ya nchi hiyo ni Waislamu.
Mongolia
Taifa kubwa la Wabuddha la Mongolia halitambui sikukuu yoyote ya kitaifa karibia na msimu sikukuu za Krismasi, na Wakristo wachache wanaishi hapa.
Bali hutumia Januari 1 kila mwaka kwa sikukuu ya kitaifa, lakini wananchi pia hufanya sherehe ya siku tatu kwa Mwaka Mpya wa Lunar wa Kimongolia, unaojulikana kama Tsagaan Sar, mwanzoni mwa mwezi wa kwanza wa mwandamo.
Korea Kaskazini
Krismasi “si tukio lisilo la kawaida” nchini Korea Kaskazini, kama ilivyo ripotiwa na The Independent.
Ufafanuzi uliokithiri wa nchi wa kimabavu juu ya kutokuwepo kwa Mungu kama inavyodaiwa kuwekwa katika mafundisho ya kikomunisti umesababisha kuharamishwa kabisa kwa mambo yote ya Krismasi.
Serikali ya Korea Kaskazini inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha habari kuhusu sikukuu za kidini haziingii katika ufalme unaoitwa hermit na mtu yeyote ambaye anaonyesha dalili yoyote ya kusheherekea sikukuu hiyo hufungwa, kuteswa au kupewa adhabu ya kifo.
Soma zaidi
- Zawadi zinazowafaa wanawake sikukuu ya wapendanao
- Zawadi za kielektroniki unazoweza kumpatia umpendae msimu wa sikukuu
- Zawadi unazoweza kuwanunulia wazazi msimu wa sikukuu
Pakistan
Ikiwa na Idadi ndogo ya Wakristo nchini humo bado imesalia na ukosefu wa usalama katika kusherehekea Krismasi, kulingana na tovuti ya habari Parhlo, na kunaweza kuwa na tishio kwa maisha ya watu wanaoadhimisha Kristmasi.
Desemba 25 ni sikukuu ya kitaifa nchini Pakistan, lakini hufanyika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Muhammad Ali Jinnah, anayechukuliwa kuwa mwanzilishi wa taifa, badala ya kuzaliwa kwa Yesu.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi
Krismasi ni tukio lisilo muhimu miongoni mwa wakazi wengi wa Kiislamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi, jimbo linalotambuliwa kwa kiasi ambalo linadai mamlaka juu ya eneo lote la Sahara Magharibi.
Saudi Arabia
Miti ya Krismasi au kufanyika kwa sherehe zozote zinazohusiana na Krismasi zilipigwa marufuku kwa miaka mingi nchini Saudi Arabia.
Hata hivyo, kwa sasa mambo yameanza kubadilika ambapo miti ya Krismasi na mapambo ya kumeta yanauzwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.Mwanamfalme Mohammed Bin Salman bin Abdulaziz amedai kuwa amejitolea kuongoza ufalme huo kuelekea Uislamu ulio wazi na wa wastani na hivyo kutoa fursa kwa dini nyingine kufanya mambo yao.
Somalia
Mwaka 2015, Somalia, ambayo ilipitisha sheria ya Sharia mnamo 2009, ilipiga marufuku kusherehekea Krismasi moja kwa moja, ikionya kwamba sherehe kama hizo za Kikristo zinaweza kutishia imani ya Kiislamu ya taifa hilo.
Tajikistan
Miaka sita iliyopita, jimbo la Tajikistan lililokuwa na watu wengi wasio na dini la Kisovieti liliharamisha miti ya Krismasi na kutoa zawadi shuleni.
“Matumizi ya fataki, milo ya sherehe, kutoa zawadi na kukusanya pesa” yalipigwa marufuku kupitia agizo lililotolewa na wizara ya elimu.
Nchini Saud Arabi, Krismas haitambuliwi lakini katika maeneo mbalimbali yamewekwa mapambo mbalimbali kuashiria sikukuu hiyo ipo. Picha| CTV News.
Tunisia
Ingawa Krismasi haijapigwa marufuku hapa, haina sherehe za kitaifa wala likizo hivyo na ni siku ya kawaida ya kazi kwa nchi.
Uzbekistan
Licha ya karibu asilimia 10 ya nchi kuwa na Wakristo wa Othodoksi ya Mashariki, Krismasi haisherehekewi hapa.
Badala yake, sherehe za Mwaka Mpya wa Uzbekistan zinafanana kwa karibu na sherehe za Krismasi, kamili na miti na kubadilishana zawadi. Hata hivyo, ni likizo ya kidunia.
Yemen
Nchi iliyokumbwa na vita ya Yemen haijaadhimisha rasmi Krismasi kwa miongo kadhaa. Mwaka jana Desemba 25, raia wa Yemeni katika kitongoji cha Al-Jahmiliya waliwasha “mamia ya mishumaa” tarehe 25 Disemba, “kuvuta hisia za ulimwengu” kumaliza vita katika mji wao wa Taez.
Hata hivyo, Krismasi haitambuliwi kabisa.
Uchambuzi huu umefanywa na waandishi wa habari Wilson Malima na Maria Acley.
Latest