Mvua, upepo wasimamisha usafiri wa vivuko Ziwa Victoria

January 18, 2022 1:19 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vivuko vinavyofanya safari Kigongo-Busisi mkoani Mwanza.
  • Serikali yasema hali itarejea kama kawaida mvua ikipungua.

Mwanza. Wasafiri wanaopita katika barabara ya Kigongo-Busisi inayokatiza Ziwa Victoria mkoani Mwanza wamelazimika kutumia muda mrefu kuvuka kwenye kivuko hicho huku sababu ikitajwa kuwa ni kuwepo kwa mawimbi makali  ziwani yaliyosababisha vivuko viwili kutofanya kazi. 

Eneo la  Kigongo-Busisi kuna vivuko vitatu vinavyofanya kazi ya kuvusha abiria,  mizigo na magari ambavyo ni MV Sengerema,  Mv Mwanza na Mv Misungwi.

Wakizungumza na Nukta habari leo Januari 18 baadhi ya abiria waliofika kivukoni hapo wamesema wamekuta kivuko kimoja tu kukifanya kazi. 

“Hatujui tatizo ni nini tumefika hapa toka saa 9 alasiri (Januari 17, 2022) tukakuta foleni ndefu hadi saivi saa 4 usiku bado hatujavuka, ” amesema mmoja wa wasafiri aliyejitambulisha kwa jina la Aloyce Kusekwa

Kusekwa ameiomba Serikali kama kuna tatizo kivukoni ni vema matangazo yawe yanatolewa ili kuondoa usumbufu kwa kuwa wapo watu wanaharaka na wengine wanarudisha watoto shule. 

Amesema changamoto hiyo imesababisha baadhi ya abiria kugeuza magari kwenda kuvuka upande mwingine wa Kamanga.


 Soma zaidi: 


Akizungumza changamoto hiyo, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Temesa Mkoa wa Mwanza, Hassan Karonda amesema amezungumza na mkuu wa kivuko hicho na kueleza kuwa hali hiyo imesababishwa na uwepo wa mvua kubwa eneo hilo iliyoambatana na upepo mkali.  

Amewatoa wasiwasi wasafiri kuwa hali ya usafiri itarejea kawaida mawimbi yakitulia.

” Hadi sasa eneo la Kigongo Busisi kuna mvua kubwa na mawimbi makali hali ikitulia usafiri utarejea kama kawaida, ” amesema Karonda.

Pamoja na sababu hizo huenda kukamilika kwa daraja linaloendelea kujengwa kwenye kivuko hicho kutaondoa changamoto ya wasafiri kutumia muda mrefu kusubiri kivuko kwenda upande wa pili.

Kwa sasa wasafiri wanalazimika kutumia takribani dakika 15 hadi 30 wakiwa wanasubiri kuvuka. 

Ujenzi wa daraja la JPM  ambao unagharimu zaidi ya Sh699 bilioni kwa sasa umefikia asilimia 34 na unatarajiwa kukamilika February  2024.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV