Muhimbili yakanusha kuwafuta kazi wafanyakazi 200

September 25, 2025 2:49 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema ililazimika kusitisha mikataba ya muda mfupi kwa wafanyakazi 27 waliokuwa wakihudumu kwa kujitolea baada ya kupata wafanyakazi wapya.

Dar es Salaam. Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa hospitali hiyo imewafukuza kazi wafanyakazi 200 kutokana na ukosefu wa fedha za kuwalipa mishahara.

Taarifa hizo zilizoenezwa kupitia kurasa za Instagram na Facebook, zilionyesha barua ya mmoja wa wafanyakazi aliyepewa notisi ya kusitishiwa ajira ya mkataba, jambo ambalo uongozi wa Muhimbili umeeleza siyo kweli.

Akitoa ufafanuzi, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, kwenye taarifa yake ameeleza kuwa kwa sasa Muhimbili ina jumla ya wafanyakazi 4,326, ambapo 3,193 wapo Upanga na 1,133 wapo Mloganzila.

“Kati ya hao, wafanyakazi 4,075 wana ajira za kudumu na 251 wana mikataba ya muda mfupi. Ajira za muda mfupi mara nyingi zinahusishwa na miradi mbalimbali ya hospitali, na pindi inapofikia ukomo, mikataba husitishwa kwa mujibu wa taratibu,” imeeleza taarifa hiyo. 

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa kuanzia Januari hadi Septemba 25, 2025, Muhimbili imepokea jumla ya wafanyakazi 380 wapya wa kudumu, na kutokana na ongezeko hilo, hospitali ililazimika kusitisha mikataba ya muda mfupi kwa wafanyakazi 27 waliokuwa wakihudumu kwa kujitolea ‘volunteers’.

“Hivyo basi, taarifa kuwa hospitali imesitisha ajira za wafanyakazi 200 siyo za kweli. Tunapenda kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo za upotoshaji,” amesisitiza Aligaesha kwenye taarifa yake.

Uongozi wa Muhimbili umesema kuwa utaendelea kuajiri na kusitisha ajira pale inapobidi, kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

Nukta TV