Serikali yamwaga ajira zaidi ya 21,000 za watumishi wa afya, elimu
- Rais Samia ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa kada za ualimu na afya, jambo likalosaidia kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hizo nyeti nchini.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa kada za ualimu na afya, jambo likalosaidia kupunguza uhaba wa watumishi katika sekta hizo nyeti nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki katika taarifa yake iliyotolewa leo Aprili 12, 2023 amesema kati ya watumishi hao, 13,130 ni walimu wa sekondari na msingi na waliobaki ni watumishi wa afya watakaofanya kazi katika hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati.
Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa ktk Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha ktk shule za Msingi na Sekondari. Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauro, Vituo vya Afya na Zahanati” @AngellahKairuki
pic.twitter.com/HvjM8H7bpB— OFISI YA RAIS TAMISEMI (@ortamisemitz) April 12, 2023