Mrithi wa Joshua Nassari Arumeru apata ‘kigugumizi’ kuuliza swali bungeni

May 22, 2019 9:19 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Amejikuta akiipoteza fursa ya kuuliza swali kwa mara ya kwanza baada ya kupewa nafasi na kuishia tu kutoa shukrani kwa kupata nafasi ya ubunge.  
  • Wabunge wasema ni mgeni, yeye awaambia wamsubiri ajipange kidogo.

Dar es Salaam. Mbunge mpya wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Dk John Pallangyo aliyeapishwa leo bungeni amejikuta akiipoteza fursa ya kuuliza swali bungeni kwa mara ya kwanza baada ya kupewa nafasi ya kufanya hivyo na Spika Job Ndugai na kuishia tu kutoa shukrani kwa kupata nafasi ya ubunge.  

Mbunge huyo amechukua nafasi ya Joshua Nassari aliyepoteza sifa ya kuwa Mbunge Machi mwaka huu kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge. 

Kwa kawaida wabunge wengi hutumia ipasavyo nafasi ya kuuliza maswali bungeni ili kupata majibu ya matatizo yanayowakabili wapiga kura wao. Kuna wakati Spika hukatisha maswali kutoka kwa wabunge baada ya kipindi cha maswali na majibu kukamilika kutokana na kuwepo utitiri wa maswali. 

Baada ya Spika Ndugai kumpa nafasi kuuliza swali la nyongeza katika Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa kijiji cha Ngalinanyuki na hifadhi ya Taifa ya Arusha, Dk Pallangyo hakujielekeza moja kwa moja katika swali lake zaidi ya kumshukuru Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya katika Taifa.

“Mheshimiwa Spika na mimi nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nisimame mbele ya Bunge lako Tukufu leo kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yangu.

“Nichukue nafasi hii basi kumshukuru Mungu sana kwa uhai na kutukutanisha leo lakini kwa kunipa nafasi hii ya kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza katika jimbo la Arumeru Mashariki. 

“Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Spika….Mheshimiwa Spika nilikuwa nimejiandaa kuuliza swali kwenye maji. Namshukuru sana na kumpongeza Rais wetu Dk John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya,” amesema Dk Pallangyo huku wabunge wenzie wakisikika nyuma wakisema “huyu ni mgeni”. 


Zinazohusiana:


Wakati Pallangyo akiendelea kuongea, Spika Ndugai alimkatisha na kusema, “asante sana Mhe Pallangyo na utauliza swali hilo wakati mwingine nilifikiri una swali katika eneo la Momella.” 

Lakini akasikika tena Mbunge huyo akisema, “Waheshimiwa Wabunge nisubirini kidogo nijipange.” 

Baada ya hapo, Spika akamwambia akae chini ili waendelee na maswali ya wizara nyingine. 

Awali swali hilo liliulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige  ambapo amesema Serikali haioni ni wakati mwafaka kuwa yeye na Mbunge aliyeapishwa leo (Dk Pallangyo) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla waende mpaka Kijiji cha Ngalinanyuki kwenda kuwasikiliza wananchi wa kijiji hicho ili kero yao ifikie mwafaka?

Akijibu swali hilo, Dk Kigwangalla amesema mgogoro katika eneo hilo la Momella haupo kwa sababu ulimalizwa mahakamani lakini amemwagiza Naibu Waziri wa wizara yake, Constantine Kanyasu aongozane pamoja na wabunge hao kwenda kuongea na wananchi wa eneo hilo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV