Mchango wa uandishi wa habari za takwimu katika uchumi wa kidijitali

December 20, 2021 6:07 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Unaanza na takwimu kutumika kwa ajili ya maendeleo.
  • Kupitia takwimu,wafanyabiashara wanaweza kujua tabia za wateja wao.
  • Takwimu pia zinasaidia kufahamu vitu vya kupewa vipaumbele.

Dar es Salaam. Matumizi ya takwimu yanazidi kuongezeka kadiri teknolojia inavyozidi kukua. Katika dunia ya leo, simu janja zimekuwa chanzo kikubwa cha kukusanya taarifa za watu na vitu.

Taarifa za makazi na jiografia ni kati ya taarifa ambazo watu huzijaza katika simu zao na wakati mwingine bila hata kujua au kuzipa umuhimu.

Mathalan, takwimu za umri, makazi hasa tunazopakia mtandaoni zimekuwa zikitumika na wafanyabiashara kutuletea matangazo na hata maudhui unayokutana nayo mtandaoni.

Mlundikano wa takwimu hizo, unatoa sababu za kubadilisha jinsi ya kufanya biashara na kujielekeza katika uchumi wa kidijitali ili kukidhi mahitaji ya kila mlaji.

Mkurugenzi wa kampuni ya Nukta Africa inayomiliki tovuti ya Nukta Habari (www.nukta.co.tz) Nuzulack Dausen amesema uwepo wa takwimu nyingi umebadilisha namna ya kuandaa na kusambaza habari.

Wadau wa takwimu wakizungumza katika mjadala wa mchango wa uandishi wa habari za takwimu katika maendeleo ya uchumi wa kdijitali Tanzania katika tamasha la data jana Desemba 7, 2021. Picha| Data Tamasha.

Dausen aliyekuwa akizungumza katika mjadala wa tamasha la data uliofanyika leo Desemba 7, 2021 jijini Dar es Salaam amesema, zamani ilikuwa ni kusubiri matangazo ya televisheni na redio lakini kwa sasa mambo yamebadilika kiasi cha wananchi kuwa vyanzo vya habari kwa vyombo vya habari.

Hilo pia linabadilisha utendaji kazi wa vyombo vya habari kutoka kuripoti hadi kufanya uchambuzi na kutoa maana ya takwimu zilizopo.

“Tuliwahi kuwa na kipengele cha bei ya mazao ambacho timu yetu ilikuwa inachakata bei za mazao ya muhimu kutoka kwenye seti ya takwimu nyingi. Tulivyoacha kutengeneza tulianza kupokea simu za watu wakiulizia,” amesema Dausen.

Mdau huyo wa takwimu ameeleza kuwa takwimu zinasaidia kufanya maamuzi ya maendeleo, miradi na biashara. 

Takwimu zinatenga mbivu na mbichi

Mlundikano wa takwimu unaweza usionekane kuwa na umuhimu kwa baadhi ya watu lakini kwa wafanyabishara na wafanya maamuzi, takwimu zinasaidia kuonyesha vitu muhimu kwa watoa huduma na mahitaji ya wateja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu ameeleza kwenye mjadala huo kuwa, uwepo wa takwimu unachochea waandishi wa habari kuibua njia mpya za kuandaa habari zao ili ziwasaidie walaji kufanya maamuzi. 

Mdau huyo wa habari amesema, takwimu zinasaidia kutengeneza agenda na kuandaa habari ambazo zimethibitishwa.

“Tunatumiaje takwimu kuchochea uwajibikaji katika uchumi wa kidijitali? Takwimu zinatupatia nafasi ya kufanya uthibitishaji wa habari kwani uwepo wa takwimu nyingi pia ni mwanya wa uwepo wa habari za uongo,” amesema Machumu.


Soma zaidi


Takwimu na hadhira

Takwimu husaidia kuwaelewa wateja wako na watu unaowahudumia mtandaoni ili kuwapatia bidhaa na huduma wanazostahili.

Kuanzia kitu ambacho wateja wanakipenda zaidi hadi vitu ambavyo watu hawana mpango navyo.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya habari na teknolojia ya Ona Stories, Tulanana Bohela amesema kwa kampuni ambazo zinatumia mitandao ya kijamii takwimu zinaweza kuwasaidia kujua njia za kuandaa maudhui yao.

“Tunahama kutoka kwenye zama za habari za maneno na maandishi na kuingia kwenye zama za habari picha (visual),” amesema Bohela.

Bohela amesema kupitia takwimu za mitandao ya kijamii itawasaidia watengeneza maudhui kujua njia za kuandaa maudhui hayo pamoja na muundo unaofaa.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV