Mbinu zitakazokusaidia kutimiza malengo wakati ukiukabili mwaka mpya

December 26, 2018 2:55 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Panga vizuri malengo machache yanayoeleweka ili kila unachokifanya kisaidie kukamilisha malengo hayo.
  • Bidii ya kazi na uvumilivu ni silaha ya kufanikiwa na kuyashinda matatizo.
  • Epuka kupoteza muda wako kwa vitu visivyo vya msingi.

Zimebaki siku chache tuingie mwaka mpya wa 2019. Ni muda ambao wengi wameanza kujiwekea mipango mbalimbali na kuboresha maisha yao kuelekea kilele cha mafanikio ya kweli.

Kwa kuwa Nukta tunakupa yale yanayokuhusu, tunakuletea njia unazoweza kuzitumia ili kuhakikisha mwaka mpya unakuwa bora kwako.


Panga malengo yako vizuri

Kama lengo lako ni kununua gari katika mwaka ujao basi hakikisha unavyovifanya vinazunguka eneo hilo, sio unataka kununua gari kila mtu akikwambia gari fulani zuri basi na wewe unaenda, haitakiwi kuwa hivyo. Chagua unalolipenda na nguvu zako za kuweka pesa zijikite katika kununua gari hilo.

Ikiwa unataka kupungua uzito basi weka malengo yako vizuri, tafuta njia za kufanya kupunguza uzito kwa kuanza ‘diet’ au kufanya mazoezi. Na unatakiwa ukaze bila kuyumbishwa na mtu au kushawishika kwa namna moja au nyingine kutoka kwenye  lengo lako.


Zinazohusiana: 


Usiridhike na maisha uliyonayo

Ongeza juhudi kuhakikisha unakuwa na umakini kwa vitu unavyovifanya, hii ni pamoja na kutokukubali kubaki hapoulipo. Pindi unaporidhika umakini wa kufanya kazi unapotea na wataalam wa saikolojiawanasema kuwa binadamu ana tabia ya kuridhika mapema akifika hatua fulani ya kimaisha, jambo linaloweza kuleta matokeo hasi.

Upousemi unaosema nitalala uzeeni,una maana kuwa fanya kazi kwa bidii wakati ukiwa na nguvu ili kujiandaa na maisha mazuri zaidi ya uzeeni wakati ambao uwezo wa kufanya kazi unakuwa umepungua.

Matajiri kama Mohamed Dewji, Reginald Mengi na Bill Gates bado wanafanya kazi na kuwekeza kila wanapopata fursa licha ya utajiri walionao ambapo wanaweza kukaa na kupumzika lakini bado wanatafuta hatma ya maisha yao.

Kuwa Mvumilivu

Hakuna kitu utakipata kwa wakati unaoutaka ni Mungu anayepanga lakini inapaswa na wewe ujiongeze kwa kuonyesha uvumilivu wa hali ya juu, kwani kila kipindi katika maisha ya binadamu ni cha mpito.

Wataalam wa saikolojia kutoka mtandao wa Psychological Todaynchini Marekani wanasema kuwa wakati ukipitia kipindi kigumu ni wakati ambao uvumilivuunafunguanjia ya kutafakari na kuzikabili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Hakikisha unapanga muda wa kuingia katika mitandao ya kijamii, kuangalia TV, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ili usiingiliane na shughuli muhimu za uzalishaji mali. Picha| Pinterest

 

Shirikisha watu wako wa karibu

Washirikisherafiki au ndugu zako kuhusu malengo yako wanaweza kukupa ushauri au njia za kufikia, lakini unatakiwa kuchagua wachache ambao wataweza kukuelekeza njia za sahihi kulingana na uelewa wao.

Kumbuka hapa unatakiwa kuwa makini sio wote wanaopenda maendeleo yako hivyo akili iwe kichwani kwako na wapo watakaokukatisha tamaa ila unatakiwa usiyumbishwe na mtu.


Epuka kupoteza muda kwa vitu visivyo vya msingi

Epuka vitu vyote vilivyokukwamisha katika kufikia malengo yako ya mwaka2018.  Piani wakati sahihi wa kuachana na watu wanaokupotezea muda (‘Time Stealers’

Hakikisha unapanga muda wa kuingia katika mitandao ya kijamii, kuangalia TV, kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ili usiingiliane na shughuli muhimu za uzalishaji mali.

Hii itakusaidia kufika mbali kimaendeleo na achana na watu ambaohawachangii kukua kitaaluma au kimaisha.

Kumbuka haya yote yanatakiwa yanakamilishwa na heshima ya muda na kujali afya yako, kwasababu bila ya hivi vitu viwili utakuwa unarudi palepale ulipotoka.

Tunakutakiwa heri ya mwaka mpya tunaamini utaendelea kuchagua njia sahihi ya maisha na sisi tutaendelea kukupa yanayokuhusu.

Enable Notifications OK No thanks