Maumivu: Wawekezaji benki ya KCB soko la hisa Dar

December 10, 2019 1:26 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Thamani ya hisa zake zimeshuka kwa asilimia 0.86 na kuwafanya wawekezaji wake wapoteze Sh10 kwa kila hisa moja.
  • Kampuni nyingine iliyopoteza leo ni ya habari ya NMG ambayo thamani ya hisa zake imeshuka kwa asilimia 2.25.

Dar es Salaam. Wawekezaji wa kampuni mbili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwemo benki ya KCB leo watalala na maumivu baada ya thamani ya hisa za kampuni hizo kushuka kwa viwango tofauti ikilinganishwa na ijumaa ya Desemba 6, 2019.

Wiki za DSE hujumuisha siku za kazi pekee yaani Jumatatu hadi Ijumaa.

Ripoti ya soko ya siku ya DSE ya Desemba 10 inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa jioni ya leo kampuni ya habari ya NMG ndiyo iliyofanya vibaya zaidi baada ya thamani ya hisa zake kushuka kwa asilimia 2.25 ambapo wawekezaji wake wamepoteza Sh20 kwa kila hisa moja. 

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa thamani ya hisa moja ya NMG ilikuwa Sh870 kutoka Sh890 iliyorekodiwa ijumaa. 

Kampuni nyingine ambayo thamani ya hisa zake imeshuka ni benki ya KCB ambayo thamani ya hisa zake zimeshuka kwa asilimia 0.86 na kuwafanya wawekezaji wake wapoteze Sh10 kwa kila hisa moja. 

Zinazohusiana: 

Wakati wawekezaji wa kampuni hizo wakiugulia maumivu, hakuna hata kampuni moja ambayo thamani ya hisa zake imepanda katika soko hilo huku nyingi zikibaki katika viwango vilivyokuwepo ijumaa zikiwemo Vodacom na benki ya CRDB, DCB na Acacia. 

Hata hivyo, benki ya CRDB ndiyo iliyofanya vizuri zaidi leo sokoni baada ya kampuni hiyo kuongoza kwa kuuza kiwango kikubwa cha hisa. 

CRDB imeuza hisa 1.2 milioni sawa na asilimia 99.9 ya hisa zote zilizouzwa sokoni leo huku ikifuatiwa kwa mbali na kampuni ya TPCC ambayo imeuza hisa 880 na DSE (10).

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

🔴LIVE: RAIS SAMIA AKIHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU, UONGOZI DARAJA LA PILI KOZI 2025/26

Nukta TV

Rais Samia: Anzisheni mfuko  kuwasaidia wafungwa wenye ujuzi wanapotoka gerezani