Maumivu kwa wawekezaji Acacia, Kenya Airways soko la hisa Dar
Kenya Airways na Acacia wameungana na benki ya KCB katika maumivu hayo ambapo thamani ya hisa zake imeshuka kwa asilimia 1.15 hadi kufikia Sh860 kutoka Sh870 ya jana. Picha|Mtandao.
- Thamani ya hisa za kampuni hizo zimeshuka kwa viwango tofauti.Â
- Wawekezaji wa Kenya Airways wamepoteza Sh5 huku wa Acacia wakipoteza Sh200 kwa kila hisa moja iliyouzwa sokoni.Â
- Wawekezaji wa kampuni ya habari ya NMG na NICO wao ni kicheko tu.Â
- Benki ya CRDB yaongoza kuuza hisa nyingi kwa asilimia 81.02.
Dar es Salaam. Wawekezaji wa kampuni za Acacia (ACA), Kenya Airways na benki ya KCB katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) leo watalala na maumivu baada ya thamani ya hisa za kampuni zao kushuka kwa viwango tofauti kutoka viwango vya jana Juni 26, 2019.
Kenya Airways ndiyo kampuni iliyofanya vibaya zaidi leo sokoni baada ya thamani ya hisa za kampuni hiyo kushuka kwa asilimia 5.56 na kuwafanya wawekezaji wake wapoteze Sh5 kwa kila hisa moja iliyouzwa.
Ripoti ya soko ya siku ya DSE ya Juni 27 inaonyesha kuwa hadi soko linafungwa leo jioni thamani ya hisa moja ya Kenya Airways ilikuwa inauzwa kwa Sh85 kutoka Sh90 iliyorekodiwa jana.
Nao wawekezaji wa kampuni ya Acacia (ACA) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) leo watalala na maumivu baada ya thamani ya hisa za kampuni hiyo kushuka kwa asilimia 3.77 na kuwafanya wapoteze Sh200 kwa kila hisa moja kutoka kiwango cha jana.
Katika soko la leo, hisa moja ya Acacia ilikuwa inauzwa kwa Sh5,100 ikilinganishwa na  Sh5,300 iliyorekodiwa jana.
Kenya Airways na Acacia wameungana na benki ya KCB katika maumivu hayo ambapo thamani ya hisa zake imeshuka kwa asilimia 1.15 hadi kufikia Sh860 kutoka Sh870 ya jana.Â
Zinazohusiana:Â
- M-pesa, intaneti vyachangia Vodacom Tanzania kupata faida ya Sh90 bilioni
- Wawekezaji wa Acacia soko la hisa Dar tabasamu tupu
- Maumivu kwa wawekezaji wa kampuni ya bia soko la hisa Dar
Wakati kampuni hizo zikifanya vibaya, wawekezaji wa kampuni ya habari ya NMG na kampuni ya uwekezaji ya NICO leo watalala na tabasamu baada ya thamani ya hisa za kampuni zao kupanda kwa viwango tofauti.
Thamani ya hisa za NICO imepanda kwa asilimia 2.94 na kuwafanya wawekezaji wake waweke kibindoni Sh5 kwa kila hisa moja iliyouzwa.Â
Ripoti ya siku ya DSE inaeleza kuwa hisa moja ya NICO imeuzwa kwa Sh175 ikilinganishwa na Sh170 ya jana huku thamani ya hisa za NMG zikipanda kwa asilimia 1.89.
Wakati Kenya Airways ikiwa ndiyo kampuni iliyofanya vibaya zaidi leo sokoni, kampuni nyingi zimebaki katika viwango vilivyokuwepo jana zikiwemo Vodacom, benki ya CRDB, DCB na NMB.
Hata hivyo, CRDB ndiyo iliyoongozwa kwa kuuza hisa nyingi zinazofikia 142,855 sawa na asilimia 81.02 ya hisa zote zilizouzwa leo sokoni.Â