Mambo muhimu ya kuzingatia unapokata rufaa ya mkopo HESLB 2023 – 24

November 9, 2023 5:43 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Dirisha litakuwa wazi kwa muda wa siku sita pekee.
  • Maombi yote yanapaswa kutumwa kwa njia ya mtandao kupitia akaunti ya SIPA.

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imefungua rasmi dirisha la maombi ya rufaa kwa wanafunzi  ambao hawakupangiwa kabisa fedha katika awamu tatu zilizopita au wale ambao hawakuridhishwa na kiasi cha fedha walichopangiwa huku ikiainisha mambo muhimu ya kuzingatia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na HESLB dirisha hilo litakuwa wazi kwa siku sita kuanzia jana Novemba 8, 2023 hadi Jumatatu Novemba 13, 2023. Ambapo maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao.

Waombaji watatakiwa kuingia katika akaunti zao za SIPA, kufungua kipengele kilichoandikwa (appeal for loan) na kisha kufuata maelekezo na kujaza taarifa na nyaraka sahihi zinazohitajika.

Taarifa ambazo muombaji wa rufaa atatakiwa kujaza katika akauti ya SIPA. Pichal Esau Ng’umbi/Nukta

Aidha, wanafunzi wamekumbushwa kuzingatia muda wa kukata rufaa wa siku sita uliowekwa ili maombi yao yaweze kuchakatwa kwa wakati.

Itakumbukwa kuwa Serikali ilitenga Sh731 bilioni kwa ajili ya  wanafunzi 220,376 kwa mwaka wa masomo 2023/2024. Kati yao wanafunzi 75,000 wanatarajiwa kuwa ni wanufaika wa mwaka wa kwanza baada ya kukamilishwa kwa uchambuzi wa maombi ya rufaa yatakayowasilishwa.

Mpaka Novemba 2, 2023 Idadi ya wanafunzi wapya waliopangiwa mikopo ilifikia  73,078 baada ya kutangazwa kwa awamu ya tatu ya wanufaika 2,518 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 6.9 bilioni.

Awali wanafunzi 56,132 wa shahada ya kwanza walipangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 159.7 bilioni katika awamu ya Kwanza iliyotangazwa Ijumaa, Oktoba 20, 2023 ikifuatiwa na awamu ya pili iliyokuwa na wanafunzi 14,428 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 44.2 bilioni iliyotangazwa Ijumaa, Oktoba 27, 2023.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
3 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
3 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Msikie Jaji Mkuu Masaju : Mambo wasiopaswa kufanya madalali wa Mahakama.

Nukta TV

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Dk Mwigulu: Kama siyo Rais Magufuli mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere usingefanyika

Nukta TV

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Umuhimu wa elimu ya mikopo

Nukta TV