Mambo atakayoshuhudia Samia tamasha la utamaduni Mwanza

September 6, 2021 11:00 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la utamaduni.
  • Atapata fursa ya kushuhudia matukio mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.
  •  Litafanyika kwa siku mbili kati ya Septemba 7 na 8 mwaka huu katika viwanja vya Red Cross, Kisesa wilayani Magu.

Mwanza. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la utamaduni litakalofanyika mkoani Mwanza na atapata fursa ya kushuhudia matukio mbalimbali ikiwemo ngoma za asili za makabila ya Kanda ya Ziwa.

Tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili kati ya Septemba 7 na 8 mwaka huu katika viwanja vya Red Cross, Kisesa wilayani Magu.

Miongozi mwa mambo yatakayofanyika kwenye tamasha hilo ni pamoja na michezo ya jadi kama kurusha mkuki , kucheza bao, kucheza na mti, uandaaji wa chakula kwa njia ya asili na kuandaa moto bila kutumia kiberti (kupekecha).

Pia ngoma za asili za makabila mbalimbali pamoja na namna ya kusimika viongozi wa kimila itakuwa ni miongoni mwa burudani ambazo Rais Samia anatarajia 

Katibu wa Umoja wa Machifu wa Kisukuma, Aaron Mikomangwa amesema tamasha hilo linatarajiwa kukusanya machifu zaidi ya 120 kutoka sehemu mbalimbali nchini.

“Katika tamasha hili tutashuhudia mambo kadhaa ya kiutamadauni ikiwemo suala la mavazi, michezo ya jadi, utamaduni wa namna ya kuwasimika viongozi wa makabila na ngoma pamoja na kuona namna akina mama walivyokuwa wakitwanga mpunga kwa kutumia michi mitatu kwenye kinu moja,” amesema Mikomangwa.

Katika  tamasha hilo watu watapata fursa ya kuona na kuzungumzia tamaduni zilizo kwenye maeneo yao na uhusiano wake na kijamii ikiwa ni sehemu ya alama mhimu kwa Mtanzania.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV