Rais Samia kushiriki tamasha la utamaduni (Bulabo), Mwanza

June 9, 2023 8:21 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni tamasha la utamaduni wa Wasukuma ambalo hufanyika msimu wa mavuno.
  • Ni sehemu ya kutangaza mila, desturi pamoja na utalii wa utamaduni.
  • Atatembelea miradi ya kimkakati kufatilia maendeleo yake.

Mwanza. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara kikazi mkoani Mwanza kwa siku tatu ambapo atashiriki uzinduzi wa tamasha la Bulabo pamoja na kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani humo.

Bulabo ni tamasha la utamaduni la wasukuma ambalo hufanyika kila mwaka msimu wa mavuno unapowadia ambapo huandaliwa na kituo cha utamaduni cha Bujora pamoja na Watemi wa koo mbalimbali za kisukuma ambapo kwa mwaka 2023 litafanyika Kisesa katika Wilaya ya Magu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla aliyekuwa akizungumza na wakuu wa taasisi zinazosimamia miradi ya mkakati jana Juni 8 2023, amewaambia Rais Samia atawasili Juni 12 ambapo Juni 13 atazindua tamasha hilo na Juni 14 atatembelea miradi.

“Chifu Hangaya anarudi kule alipopewa uchifu, hivyo tutakuwa na tamasha kubwa, maandalizi yanaendelea na yapo katika hatua nzuri. Juni 14 katika Mkoa wetu Rais atapita katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kufuatilia mradi wa Kigongo-Busisi, mradi wa ujenzi wa meli ya Mv Mwanza pamoja na hoteli ya NSSF,” amesema Makalla.

Septemba 8, 2021 Rais Samia alisimikwa kuwa Mkuu wa Machifu Tanzania Mkoani Mwanza wakati akifunga Tamasha la Utamaduni lililoandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania.


Soma zaidi


Pamoja na kutawazwa kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote nchini, Rais Samia alipewa  jina la Chifu Hangaya likiwa na maana ya Nyota ya asubuhi inayong’aa.

Kwa mujibu wa Rais Samia Utamaduni hutangaza mila na desturi za nchi lakini pia ni biashara na chanzo kikubwa cha mapato kwasababu ni moja ya vivutio vya utalii.

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023/24 imepanga kuboresha utalii wa utamaduni pamoja na matarajio ya kupata jumla ya watalii 63,519 na mapato ya wastani wa Sh265.5 milioni. 

Pamoja na kushiriki katika uzinduzi wa tamasha hilo Rais Samia atatembelea baadhi ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani Mwanza ya ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2 pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.