Malengo: Ngazi ya kukufikisha katika ndoto zako
- Mipango iko kwenye kila jambo unalolifanya hata kama ni dogo kiasi gani.
- Anza leo kupanga kuhusu mustakabali wa baadaye wa maisha yako.
Dar es Salaam. Kupanga ni kuchagua. Na uchaguzi unategemea anayepanga anataka nini kwenye maisha yake. Mipango iko kwenye kila jambo unalolifanya hata kama ni dogo kiasi gani.Â
Mathalan, unapotaka kutoka nyumbani asubuhi ni lazima utajipanga utoke vipi kwa maana utachagua nguo nzuri ambayo unaamini itakufaa kwa siku hiyo. Hapo umepanga mipango.
Hata wewe kijana unayesoma makala hii, unatakiwa kuwa na mipango iliyojitosheleza kuhusu maisha yako. Usisubiri kufika ngazi fulani ya maisha. Anza leo kupanga kuhusu mustakabali wa baadaye wa maisha yako.
Labda nikuambie tu, mipango siyo kitu cha ajabu ambacho kinatakiwa kufanya na watu fulani. Ni suala la kila mtu. Mipango ni  maamuzi ya makusudi  ambayo mtu anajiwekea ili kutimiza  jambo akitarajia kupata matokeo fulani.
Kuna ulazima wa kuwa na mipango? Ndiyo kwa sababu usipojipanga watakupanga watu wengine kwenye maisha yako. Ukiwa na mipango una nafasi kubwa ya kuboresha maisha yako:
Ni ramani ya kukuongoza
Ukiwa na mipango yako binafsi ni kama umejitengenezea ramani yako mwenyewe ambayo unatakiwa kupita kufika unakokwenda.
Hii itakusaidia kuepuka vitu visivyo na maana kwenye maisha na kukufanya utazame mambo ya msingi yenye manufaa kwenye maisha. Ramani itakulazimisha kutumia muda na rasilimali fedha vizuri.Â
                Â
Hutayumbishwa na chochote
Watu wenye mipango hawayumbishwi na chochote kwenye jamii kwa sababu wanatambua nafasi waliyonayo. Utakuja kila namna ya upepo wa mitindo na mifumo isiyo rafiki, wao watabaki kwenye msimamo walionao.
Kuna mambo yanakuyumbisha kwenye jamii? Huna mipango. Anza kupangilia mambo yako ili usipangwe na watu wengine.Â
Soma zaidi:Â
- bajeti inavyookoa matumizi mabaya ya pesa ngazi ya familia
- Jinsi ya kudhibiti matumizi mabaya ya pesa zakoÂ
- Zingatia haya wakati ukifanya manunuzi msimu wa sikukuu
Utajenga uaminifu
Miapngo inajenga uaminifu kwa wanaokuzuguka. Matokeo mazuri kwenye kazi au biashara yanayotokana na mipango ambayo itakufanya uaminiwe na watu unaofanya nao kazi.Â
Unataka kuanza leo? Basi hujachelewa tafakari kuhusu maisha yako na pangilia kila jambo unalofanya kwenye maisha yako. Â Â
Hadi wakati  mwingine tukutane tena hapa hapa katika kipindi chako cha mimi na wewe tuzungumze zaidi. Â
Neema Simbo ni mjasiriamali na mwandishi wa vitabu. Unaweza kuwasiliana naye kwa namba ya simu: +255 763 009 933 au Instagram: @eden_kush
Latest
