Makosa ya kuepuka wakati wa kufua nguo zako
- Makosa hayo ni pamoja na kufua nguo kwa sabuni nyingi ya unga na kutumia jiki kila wakati.
- Pia kufua nguo za rangi tofauti kwa wakati mmoja.Â
- Kama nguo zako hazijachafuka sana, siyo lazima uzifue, vaa tena.
Kila mtu ana nguo zake ambavyo zinazoshikilia kumbukumbu nyingi, asingependa nguo hizo zipauke au kuchakaa mapema.
Hata hivyo, kutokana na nguo hizo kuvaliwa mara kwa mara inasababisha zipoteza mng’ao wake na hivyo kukosa mvuto tena.
Inahuzunisha kuona shati au nguo yoyote uliyopewa na umpendaye kama zawadi au iliyogharamia pesa nyingi kuinunua haikuvutii tena kuivaa kutokana na kuchakaa mapema.
Baada ya dondoo za simu, magari na hata za vifaa vya kielektroniki vya jikoni, haya ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuongeza maisha ya nguo zako na kulitunza lile shati linalobeba kumbukumbu muhimu.
- Punguza matumizi ya sabuni ya unga
Nitafuaje? Najua hilo ni swali lililogonga kichwa chako baada ya kusoma dondoo hii lakini ni vizuri kutambua kuwa, kutumia sabuni nyingi wakati wa kufua siyo kutakatisha nguo.
Kulingana na malighafi zilizotengeneza nguo yako, unatakiwa kutumia kiasi stahiki cha sabuni ya unga kufulia ili kuendelea kufurahia mg’ao wa nguo zako.
Sabuni ya unga inaweza kupausha nguo zako endapo itatumika kwa wingi na hasa kwa nguo nyepesi. Cha kufanya ni kupunguza kiasi cha sabuni unachotumia na ongeza sabuni kidogo kidogo wakati unaendelea kufua.
Hata hivyo, kama nguo zako hazijachafuka sana na haukuwa na heka heka nyingi ulipozivaa, hakuna haja ya kuzifua kwani kurudia nguo siyo dhambi. Picha|Mtandao.
- Usitumie jiki kila wakati
Jiki (Bleach) Â ni moja ya malighafi vinavyoaminika kutoa madoa sugu ambayo sabuni nyingine zimeshindwa kuyaondoa.Â
Kwa mujibu wa mtandao wa RealSimple.com hauhitaji jiki kuondoa kila aina ya madoa yakiwemo damu na vitu vyote vyenye protini. Ndiyo hata mchuzi wa nyama hauhitaji jiki kutoka.Â
Unachohitaji ni sufuria, nguo zako, maji na vipande vya limao. Chemsha nguo zako kwa muda na madoa hutayaona tena.Â
Mwanafunzi Witness Sosoma kutoka Shule ya Sekondari Kifungilo iliyopo mkoani Morogoro ambaye amefundishwa stadi za kazi amesema kama una uwezo wa kufua nguo iliyopata madoa kabla hayajakauka, ni heri ufanye hivyo kwani itaondoa madoa hayo kabla hayajawa sugu.
Zinazohusiana:Â
- Jinsi ya kufanya mitandao ya kijamii isikuharibie mahusiano yako
- Â Utaoa, utaolewa lini: Jinsi unavyoweza kukabiliana na msukumo wa nje wa ndoa
- Mambo ya kufanya wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka
- Fua nguo zako za rangi nje ndani
Jifikirie namna unavyofikicha nguo wakati wa kufua. Bila shaka unatumia nguvu nyingi kutaka nguo yako iwe safi lakini kwa kufanya hivyo, unaipausha nguo yako kama ni ya rangi yenye jamii za weusi.
Inashauriwa kufua nguo zako za namna hii kwa kuzigeuza nje ndani ili kuepuka kuzipausha na hivyo kukupatia nafasi ya kufurahia mng’ao wake kwa muda mrefu.
Hata hivyo, kama nguo zako hazijachafuka sana na haukuwa na heka heka nyingi ulipozivaa, hakuna haja ya kuzifua kwani kurudia nguo siyo dhambi.
- Epuka kufua nguo nyingi kwa wakati mmoja
Kwanini utengeneze kachumbari ya nguo zako wakati wa kufua? Njano, nyekundu, nyeusi na nyeupe zote kwenye beseni moja? Hapana.Â
Unashauriwa kabla ya kufua, tenga nguo zako kwa makundi ya rangi na kisha fua kulingana na makundi hayo.Â
Kwa kufanya hivyo, itakuepushia nguo zako kuchuja wakati wa kufua na hivyo kuokoa pesa ya kununua nguo zingine.
Unashauriwa kuzinyoosha nguo zako zikiwa na unyevunyevu kwani kiasi kidogo cha maji kilichopo kwenye nguo kitakurahisishia kazi ya kunyoosha. Picha|Mtandao.Â
- Nyoosha nguo zako kwa moto stahiki
Kutokana na haraka, watu wengi hawajali kiasi cha moto kilichopo kwenye pasi wakati wa kunyoosha nguo zao.Â
Wakati pasi nyingi zikija na maelekezo ya kiasi cha moto kwa kila aina ya nguo, wengi hupuuzia.Â
Kwa kupuuza huko, unaweza kujikuta unaharibu nguo yako na kuiunguza na hivyo kupata hasara. Hujawahi ona alama ya pasi kwenye nguo? Kama bado, basi utaishuhudia hivi karibuni kwenye nguo zako endapo hautotumia moto stahiki unaopendekezwa kwa kila nguo.
Hata hivyo, unashauriwa kuzinyoosha nguo zako zikiwa na unyevunyevu kwani kiasi kidogo cha maji kilichopo kwenye nguo kitakurahisishia kazi ya kunyoosha.
Hatujamaliza bado. Zipo dondoo muhimu zinazoendelea kuja kupitia ukurasa huu. Kaa chonjo.
Latest