Magufuli afanya uteuzi Makatibu Wakuu wizara mbili

April 22, 2020 9:20 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Amemteua Prof. Mchembe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya akichukua nafasi ya Dk Zainab Chaula.
  • Dk Chaula ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.  
  • Pia Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto akichukua nafasi ya Dk Zainab Chaula ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.  

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano iliyotolewa leo (Aprili 22, 2020) inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Prof. Mchembe alikuwa Msaidizi wa Rais katika masuala ya afya.

Dk Chaula amechukua nafasi ya Katibu Mkuu wa Mawasiliano  iliyoachwa na mtangulizi wake Dk Maria Sasabo amestaafu.


Zinazohusiana


Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando na amechukua nafasi iliyoachwa na Prof. Mohamed Bakari Kambi ambaye amestaafu.

“Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 22 Aprili, 2020,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV