Magari 10 yanayotumia mafuta kidogo
- Toyota IST na Vits ni miongoni mwa magari yanayotumia mafuta kidogo.
Dar es Salaam. Huenda una ndoto ya kumiliki gari kali lenye muonekano wa kifahari, injini kubwa na nguvu barabarani. Pamoja na ndoto hiyo kubwa ila huna uhakika iwapo utaendelea kuwa na kipato cha kulihudumia muda wote.
Wasiwasi wako juu kulihudumia gari ni dhahiri kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli hususan miaka ya hivi karibuni.
Ndoto ya ‘gari la show’ inaweza kugeuka kuwa mzigo wa kila siku iwapo hatua stahiki hazitafuatwa wakati unanunua chombo chako ya moto hususan suala la mafuta na matengenezo.
Mfano, bei kikomo za mafuta kwa mwezi Mei 2026 zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) zinabainisha kuwa petroli katika Mkoa wa Dar es Salaam imepanda kwa Sh295 hadi Sh4,115 kwa lita huku dizeli ikiuzwa Sh4,248 kwa lita.
Bei hizo zimeongezeka ukilinganisha na mwezi uliopita ambapo petroli ilikuwa ikiuzwa Sh3,820 na dizeli Sh3,806 kwa lita.
Hali hii imechochewa zaidi na vita inayoendelea baina ya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Vita hiyo imeathiri mnyororo wa ugavi wa mafuta kiasi cha kupandisha bidhaa hiyo muhimu kwa kiwango kikubwa duniani kutokana na kuharibiwa kwa visima, viwanda vya kusafisha mafuta na kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz.
Wataalamu na wadau wa magari wanashauri kuwa kabla hujanunua gari, ni vema ukaangalia mahitaji yako na kipato iwapo utamudu bei ya mafuta ikiongezeka ama la.
Iwapo huna uhakika wa kipato siku za mbeleni wanashauri ununue gari lenye injini ndogo isiyotumia kiwango kikubwa cha mafuta ili kupunguza maumivu pale nishati hiyo inapopanda bei kama wakati huu.
Yafuatayo ni magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta kutokana na udogo wa injini kwa mujibu wa mafundi, waingizaji magari na tovuti za kampuni zilizotengeneza vyombo hivyo vya moto.
10. Toyota Raumu
Toyota Raum ni gari lililotengenezwa na kampuni ya Toyota ambapo matoleo mengi hutumia injini ya 1496cc (1.5L) ambayo ulaToyota Motor Corporation Official Global Websiteji wake wa mafuta ni rafiki.
Toyota Raum, iliyoanza kutengenezwa mwaka 1997 na kuhitimishwa rasmi mwaka 2011, ni gari la familia lenye nafasi kubwa ya ndani pamoja na milango ya kuvuta inayorahisisha matumizi ya kila siku.

Baadhi ya matoleo maarufu ni ‘Raum G Package’ na ‘Raum C Package’ ambayo yana uwezo wa kutumia wastani wa kilomita 14 hadi 18 kwa lita moja ya mafuta.
Gari hili linapendwa kwa kuwa na nafasi kubwa ya mizigo pamoja na uimara wa injini zake.
9.Toyota Sienta
Katika nafasi ya 9, ipo Toyota Sienta ambayo matoleo yake mengi hutumia injini ya 1496 cc (1.5L) sawa tu na Raum.
Toyota Sienta nayo ni gari la familia lenye uwezo wa kubeba kuanzia abiria watano mpaka saba kulingana na toleo pamoja na mizigo huku likiwa na matumizi mazuri ya mafuta.
Baadhi ya matoleo maarufu ni ‘Sienta X’ na ‘Sienta G’ ambayo yana uwezo wa kutumia wastani wa kilomita 14 hadi 20 kwa lita moja ya mafuta.
Gari hili linapendwa kwa nafasi kubwa ya ndani, milango ya kusukuma na ni nzuri sana kwa safari za familia.
Toleo la kwanza la Sienta lilitolewa Septemba mwaka 2003 na toleo jipya zaidi la Toyota Sienta ni la mwaka 2026 likiwa na maboresho ya muundo pamoja na teknolojia za kisasa.
Gari hili lilioanza kutengenezwa Agosti 5, 2002 na kusitishwa rasmi mwaka 2016 limekuwa maarufu sana Tanzania kutokana na uimara wake na uwezo wa kutembea vizuri hata kwenye barabara zisizo nzuri.
8.Toyota IST
Miongoni mwa magari bana matumizi yanayopigiwa upatu ni Toyota IST ni lenye muonekano wa kisasa pamoja na body imara.
Toyota IST hutumia injini tofauti kulingana na toleo la mwaka husika wakianzia na toleo la mwaka 2003 ikiwa na 1,298 cc (1.3L), 1797cc (1.5L) huku toleo la mwisho mpaka sasa likiwa la mwaka 2025.

Kwa wastani lina uwezo wa kutumia lita moja ya mafuta kwa safari ya kilomita 15 hadi 20 inategemea upo barabara kuu au mjini na hali ya matengenezo.
Mazda Demio imeendelea kupendwa kutokana na muonekano wake wa kisasa pamoja na matumizi mazuri ya mafuta.
7. Mazda Demio
Mazda Demio ni gari lililotengenezwa na kampuni ya Mazda ambapo matoleo mengi hutumia injini ya 1298cc (1.3L) huku baadhi ya matoleo mengine yakiwa na injini ya 1498cc (1.5L).
Baadhi ya matoleo maarufu ni ‘Demio 13C’ na ‘Demio Skyactiv’ ambayo yana uwezo wa kutumia lita moja ya mafuta kwa wastani wa kilomita 17 hadi 22.
6. Suzuki Swift
Suzuki Swift ni gari lililotengenezwa na Suzuki na linafahamika kwa muonekano wa kimichezo pamoja na matumizi mazuri ya mafuta.
Matoleo mengi hutumia injini ya 1197cc (1.2L) huku baadhi ya nyingine zikiwa na 1242cc hadi 1328cc kulingana na soko.
Suzuki Swift inaweza kutumia lita moja ya mafuta kwa wastani wa kilomita 18 hadi 23.
Toleo jipya zaidi la Suzuki Swift limetolewa mwaka 2024 likiwa na maboresho makubwa ya teknolojia na matumizi ya mafuta.
Gari hili lina nguvu nzuri barabarani huku likibaki kuwa chaguo linalofaa kwa matumizi ya kila siku.
5. Nissan March
Nissan March ni gari lililotengenezwa na kampuni ya Nissan ambapo matoleo mengi hutumia injini ya 998cc (1.0L) huku baadhi ya modeli zikiwa na 1198cc (1.2L) na 1240cc (1.24L).
Nissan March ilianza kutengenezwa mwaka 1982 na baadhi ya matoleo yake bado yanaendelea kuzalishwa hadi sasa katika masoko tofauti duniani.
Baadhi ya matoleo maarufu ni ‘March S’ na ‘March Bolero’ ambazo hutumia wastani wa kilomita 18 hadi 23 kwa lita moja ya mafuta.
Gari hili linapendwa kwa urahisi wa kuendesha mjini, ukubwa mdogo pamoja na gharama nafuu za matengenezo.
4. Toyota Passo
Toyota Passo ni gari lingine lililotengenezwa na kampuni ya Toyota ambayo matoleo mengi hutumia injini ya 997cc (1.0L) huku baadhi ya matoleo ya zamani yakiwa na 1297cc (1.3L).
Gari hii mpaka sasa toleo lake la mwisho ni mwaka 2015 ambapo kuna matoleo tofauti ikiwemo ‘Passo X G’ inayotumia lita moja, ‘Passo + Hana’ ambayo pia hutumia kiasi kidogo cha mafuta kwa 27.6 km/L jambo linalolifanya kuwa moja ya magari bora kwa matumizi kidogo ya mafuta.
Passo inapendwa kwa ukubwa wake mdogo, nafasi nzuri ya ndani na urahisi wa kuendesha mjini.
3. Toyota Vitz
Gari la tatu ni Toyota Vitz, hili ni gari dogo lililotengenezwa na kampuni ya Toyota nchini Japan na ni moja ya magari yenye matumizi madogo zaidi ya mafuta.
Gari hii lina matoleo (modeli ) tofauti tofauti ambapo tolea la kwanza la Vitz linatumia injini ya 997cc (1.3L) huku ya pili ikiwa na 1296cc (1.3L) ya tatu ikiwa na injini ya 1329cc.
Kulingana na toleo la gari hizi zipo zinazotumia pia mafuta hadi lita 1.5.

Gari hili lina uwezo wa kutumia wastani wa kilomita 20 hadi 26 kwa lita moja ya mafuta kutegemea tolea na mfumo wa ‘transmission’ (upitishaji).
Toleo la kwanza la gari hili lilizinduliwa Januari 13, 1999, pili Februari, 1,2005 na tatu Desemba 22, 2010.
2. Suzuki Jimny
Suzuki Jimny ni gari la pili kwa mujibu wa uchambuzi wa Nukta Tv, gari hili limetengenezwa na kampuni ya Suzuki ambapo baadhi ya matoleo yake ya soko la Japan hutumia injini ya 658cc (maarufu kama 660cc), huku matoleo mengine yakitumia 1300cc (1.3L) na 1500cc (1.5L).
Suzuki Jimny ilianza kutengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1970 na imeendelea kuzalishwa hadi leo kupitia vizazi mbalimbali vya magari hayo.
Baadhi ya matoleo maarufu yanayotumia injini ya 658cc ni Suzuki Jimny JB23 na Suzuki Jimny JB64 .
Magari hayo hutumia wastani wa kilomita 14 hadi 18 kwa lita moja ya mafuta kutegemeana na toleo na matumizi.
Suzuki Jimny linafahamika kwa uwezo mkubwa wa kwenda maeneo magumu, matumizi mazuri ya mafuta pamoja na muundo wake wa kipekee.
1. Daihatsu Mira
Daihatsu Mira ndio gari linaloshika nafasi ya kwanza katika uchambuzi wetu, gari hili lililotengenezwa na kampuni ya Daihatsu lina matoleo mengi pia hutumia injini ndogo ya 658cc (0.66L) kulingana na sheria za nchini Japan.
Daihatsu Mira ilianza kutengenezwa mwaka 1980 huku baadhi ya matoleo yake yakiendelea kutolewa hadi sasa katika masoko ya Asia.
Baadhi ya matoleo maarufu ni ‘Mira X Limited’ na ‘Mira Cocoa’ ambazo zina uwezo wa kutumia wastani wa kilomita 20 hadi 30 kwa lita moja ya mafuta.
Gari hili ni moja ya magari yenye matumizi madogo zaidi ya mafuta duniani na limekuwa maarufu kutokana na uwezo wake wa kutumia kiasi kidogo cha mafuta na muonekano wake unaofaa kwa matumizi ya mjini.
Hata hivyo, katika uchambuzi uliofanywa na Nukta TV umebaini kuwa sehemu kubwa ya magari haya ni kutoka kampuni ya Toyota.
Licha ya watalaamu hao kuelezea kuwa magari yenye injini ndogo ndio suluhu la kutumia katika kipindi hiki ambacho bei ya mafuta ipo juu, bado wamesema matengenezo ya gari mara kwa mara na uendeshaji mzuri ni muhimu ili kuimarisha matumizi ya mafuta.
Aidha, uchambuzi huu haumaanishi kuwa hakuna magari yenye injini ndogo zaidi ya haya bali unaonyesha magari ambayo ni rafiki kwa ulaji mafuta japo mengine ni madogo.
Latest