Latra yazuia mifumo minne tiketi za mabasi Tanzania

February 2, 2026 7:03 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Mifumo hiyo ni Exabytes Tiketi, Tiketi Rafiki, Safari Yetu na Safiri Tiketi.
  • Yazuiwa kwa kutofuata vigezo. 
  • Wamiliki wa mabasi wanaelekezwa kutumia mifumo ya tiketi mtandao iliyoidhinishwa peke.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imezuia mifumo minne ya ukataji tiketi mtandao kutokana na kushindwa kutimiza vigezo vya kisheria huku ikiwapa wamiliki wa mabasi muda wa siku 14 kuhamia kwenye mifumo rasmi.

Uamuzi huo wa Latra ni moja ya hatua za hivi karibuni za mamlaka hiyo kuhakikisha huduma za ukataji tiketi unafanywa mtandaoni ili kukabiliana na vishoka, ulanguzi na usumbufu kwa abiria wa mabasi wanaoshushiwa njiani. 

Kwa mujibu taarifa ya Latra, Kanuni za Tiketi Mtandao za mwaka 2024 zinataka mifumo yote ya tiketi mtandao kuthibitishwa na Latra kabla ya kuanza kutoa huduma.

Mifumo iliyopigwa marufuku na Latra ni Exabytes Tiketi unaoendeshwa na kampuni ya Exabytes Africa Ltd, Tiketi Rafiki (Global Light & Company Limited), Safari Yetu (Duarani Innovat limited) na Safiri Tiketi wa kampuni ya Itule Company Limited.

Latra imeeleza kuwa mifumo hiyo imeshindwa kurekebisha mapungufu yaliyoainishwa licha ya kupewa muda wa kutosha.

“Wamiliki wa mabasi wanaelekezwa kutumia mifumo ya tiketi mtandao iliyoidhinishwa pekee. Wasafirishaji ambao kwa sasa wameunganisha mabasi yao kwenye mifumo isiyoidhinishwa wanapewa muda wa siku 14 hadi Februari 15, 2026,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya Januari 30, 2026. 

Baada ya muda huo, mabasi hayatakuwa na ruhusa ya kutoa huduma kwa kutumia mifumo isiyoidhinishwa, huku utoaji na uhuishaji wa leseni za usafirishaji ukizingatia matumizi ya mifumo rasmi tu.

Latra pia imesisitiza umuhimu wa kutumia makondakta waliosajiliwa, watakaohakikisha kila abiria anapata tiketi ya mtandaoni kwa uwazi na urahisi katika ununuzi wa tiketi.

Hadi sasa, jumla ya mifumo 10 imekidhi vigezo na kuruhusiwa kuendelea kutoa huduma ambayo ni AB Connect, Busbora, MySafari tiketi, Iyishe, Msafiri, Baspoa, Otapp, Afritech, Voltic Tanzania na Web e-ticketing.

Kwa ambaye ana mashaka na tiketi yake, Latra  inapendekeza kutumia Latra App kuthibitisha uhalali wa tiketi na kuepuka ulanguzi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV