Kwanini uchague filamu ya “Star Wars” msimu wa sikukuu

December 20, 2019 4:57 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inaanza kuonyeshwa rasmi leo (Disemba 20, 2019).
  • Ni mfululizo wa sehemu ya sita ya filamu za Star Wars. 
  • Imejaa mafunzo lukuki yatakayokujenga mwisho wa mwaka 2019.

Dar es Salaam. Unaonaje ukiachana na makaratasi pamoja na skrini ndogo ya kompyuta yako na badala yake kuchagua skrini kubwa ya sinema kufurahia wikiendi yako?

Ndiyo, unastahili mapumziko mazuri ya mwisho wa mwaka ili kujipanga na mwaka ujao yaani 2020 ambao utaanza ndani ya siku 11 zijazo.

Furahia filamu ya “Star Wars” na nyinginezo zilizoingia sokoni katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka katika kumbi za sinema za Century Cinemax zilizopo Tanzania:

Kwanini Star wars?

Baada ya mapigano ya Crait, Kylo Ren (Daisy Ridley) anaanza safari yake kuelekea sayari ya Exegol ambapo anakutana na Palpatine ambaye anafunguka kuwa chanzo cha Snoke ambaye alikuwa ni kibaraka aliyedhamiria kumrubuni Ren ageukie upande wa “dark side” (moja ya majeshi kwenye ulimwengu wa Star Wars).

Ni kipigo juu ya kipigo, muungano baada ya muungano huku mafunzo yakiwa ni umuhimu wa kuwa na watu wa karibu ambao wapo tayari kusafiri maili moja na wewe.

Shuhudia meli za vita za angani, maji yaliyozidi kina na zaidi, unaachaje kuona jinsi “Ightsaber” (silaha za kivita za wapiganaji) zinavyoendelea kuchukua nafasi?


Zinazohusiana


Usiache kuenda na mwanao au familia kutazama filamu hii iliyogharimu takribani Sh729.4 bilioni ambayo inawakutanisha manguli kama John Boyega (Finn), Billy Williams (Lando Calris) ambaye alitisha kwenye filamu ya “Bat Man” na “Undercover Brother”.

Utaweza kuiona filamu hii imeongozwa na Jeffrey Abrams, kiongozi wa filamu zaidi ya 40 zikiwemo za “Mission Impossible” na “Overload” kwa Sh5000 siku ya Alhamis na Sh10,000 siku za wikiendi.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.