Kraken: Kirusi kipya cha Uviko-19 kinachowatesa wanasayansi

January 17, 2023 5:43 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kinatajwa kuenea kwa kasi zaidi kuliko virusi vilivyopita.
  • Uwezo wa kubadili jeni zake ni miongoni mwa sababu.
  • Barakoa yatajwa kama njia bora zaidi ya kujikinga na kirusi hicho.

Dar es Salaam. Ingawa si jambo linalozungumzwa sana kwa sasa, lakini wasiwasi unaendelea kuongezeka kwa wanayansi ambao wanajaribu kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na makali ya kirusi kipya cha Uviko-19 ambacho kinaenea kwa kasi barani Ulaya.

Kirusi hicho kinachoitwa XBB.1.5 au Kraken ni matokeo ya mabadiliko ya kijeni ya kirusi aina ya Omicron XBB ambacho nacho kiliripotiwa kuwa na kasi kubwa katika kuenea kwake.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kirusi hicho kiliripotiwa kwa mara ya kwanza Oktoba 2022, nchini Marekani na sasa tayari kimeenea katika nchi 38 barani Ulaya ikiwemo Sweden, Kanada, Australia na Ufaransa.

Disemba mwaka jana, China ilitangaza kuwa wastani wa watu 60,000 walipoteza maisha kutokana na virusi vya Omicron aina ya BA.5.2 na BF.7 vilivyozuka nchini humo.


Soma zaidi:


Mapema Januari mwaka huu Mkurugenzi wa masuala ya Teknolojia kutoka WHO, Maria Van Kerkhove alisema kirusi hicho ndiyo kinaambukiza kwa kasi zaidi kuliko aina nyingine za virusi.

“Sababu kubwa ni kutokana na kirusi hiki kuwa na uwezo wa kubadilisha jeni zake mara kwa mara hivyo si rahisi kukidhibiti,” anasema Kerkhove.

Pamoja na kwamba kirusi hichi kinaenea kwa kasi bado hakuna uhakika kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kuliko ilivyokuwa awali.

Kutokana na uwezo wa kirusi hicho kujibadili mara kwa mara kulingana na mazingira wataalamu wa afya wameshauri pamoja na chanjo ya uviko-19 njia inayotajwa kuwa na uhakika zaidi ni kuvaa barakoa muda wote mtu anapokuwa kwenye mikusanyiko.

Kwa mujibu wa Kituo Cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) mpaka sasa asilimia 43 ya visa vya maambukizi ya Uviko-19 nchini humo yamesababishwa na kirusi hicho kipya.


Tangazo


Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.