Kijana wa miaka 17 mbaroni kwa kumuua rafiki yake wakigombea mpenzi wa miaka 14

October 30, 2024 3:32 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana na wivu wa kimapenzi.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Amos Mwita (17) Mkazi wa mtaa wa Bugarika Bendera tatu kwa tuhuma za mauaji ya Daniel Kisire(18) kutokana na wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 30, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24 mwaka huu katika mtaa wa Bugarika Sokoni kata ya Mahina Jijini Mwanza ambapo marehemu aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni upande wa kushoto.

Kamanda Mutafungwa amesema tukio hilo limetokewa wakati marehemu akiwa nyumbani kwa bibi yake baada ya kuzuka ugomvi uliotokana na wivu wa kimapenzi na kusababisha kifo chake.

“Uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini, marehemu ambaye ni Daniel Kisire na mtuhumiwa ambaye Amos Mwita ni majirani ambapo marehemu alimtaka kimapenzi msichana Latifa Chombo (14) ambaye alimkatalia kisha binti huyo alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mtuhumiwa ambaye ni rafiki wa marehemu,” amesema Mutafungwa.

Mutafungwa ameongeza kuwa mara baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana na Oktoba 25 mwaka huu Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata akiwa mafichoni nyumbani kwa rafiki yake,” amesema Mutafungwa.

Kwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pamoja na mashahidi ambapo Mutafungwa amesema ushahidi utakapokamilika jalada hilo litapelekwa kwa muendesha mashtaka wa mkoa.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wakazi Jijini Mwanza wamesema ukosefu wa malezi bora kwa watoto kunachangia uwepo wa matukio hayo.

“Katika kipindi hiki ambapo wazazi wanahangaika kutafuta ridhiki wamesahau wajibu wao wamalezi hali inayosababisha watoto kujiingiza kwenye suala la mapenzi wakiwa kwenye umri mdogo,”amesema Rayond Lukas Mkazi wa Ilemela

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV