Saba mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya imani za kishirikina Mwanza

May 24, 2023 8:54 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Taratibu za kukusanya ushahidi ili kuwafikisha mahakamani zinaendelea
  • Ripoti zaonesha wanawake ndio wahanga wakubwa wa mauaji yatokanayo na imani za kishirikina

Mwanza, Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewakamata watuhumiwa saba ambao wanajihusisha na matukio ya ukatili ikiwemo mauaji kwa minajili ya kufanya vitendo vya kishirikina.

Wilbroad Mtafungwa ambaye ni Kamanda wa polisi mkoani Mwanza amebainisha kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao watatu walihusika na kupanga mauaji ya mwanamke aliyetambulika kama Ester Lukonu(51) mkazi wa Kijiji cha Bugumangala aliyeuawa kwa kukabwa shingoni kisha kukatwa sehemu za siri.

“Jeshi la polisi linapenda kuwajulisha wananchi kwamba watuhumiwa wote waliohusika katika tukio hilo walikamatwa na askari waliobobea katika upelelezi wa makosa ya jinai ambapo watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika na mauaji hayo ya kikatilii,” amesema Mtafungwa

Tukio la mauaji hayo lilitokea Mei 10 , 2023 ambapo Kwa mujibu wa Mutafungwa  kabla ya mauaji hayo marehemu alibakwa, na kisha mwili wake kutelekezwa katika shamba la mihogo.


Soma zaidi


Watuhumiwa waliokamatwa

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na  mganga anayetuhumiwa kupokea sehemu ya siri ya marehemu ambapo aliikausha kwa moto na kuisaga kwa ajili ya matumizi ya imani potofu za kishirikina.

“Vilelezo mbalimbali katika kesi hiyo vimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu,” amesema kamanda Mtafungwa

Watuhumiwa wengine ni Masunga Mabula (32) mkazi wa Nyaguge wilayani Magu, Ezekiel Mtokashegela(45)  ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Kisamba wilayani Magu na Salome Raphael (32) mkazi wa Kisamba wilayani Magu ambapo taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

Sambamba na hilo, watu wanne wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili wanandoa, Katarina Luzali(48) na Joseph Kanyasa(50) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Matale ambapo mauwaji hayo yamehusishwa baadhi ya wanakijiji kumuhisi Katarina Luzali kujihusisha  na imani za kishirikina ambapo hata hivyo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Mwanza ni miongoni mwa mikoa iliyotajwa kukiuka haki za binadamu kwenye Ripoti ya Haki za Binadamu ya Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC ya mwaka 2022.

pamoja na ripoti hiyo kubainisha kuwa matukio ya mauaji yanayotokana na imani za kishirikina yamepungua, lakini bado ni changamoto, hasa kwa wanawake, ambao ni asilimia  52 ya wahanga.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

Nukta TV