Kesi ya dereva wa basi lilioua tisa, kujeruhi Mwanza yaahirishwa hadi Novemba 11

November 5, 2024 4:32 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakimu ataja sababu ya kuahirisha kesi hiyo kuwa ni afya ya mstakiwa kutokuwa sawa.

Mwanza. Kesi inayomkabili aliyekuwa dereva wa basi la Asante rabi Shedrack Swai (37) aliyesababisha ajali na iliyoua watu tisa katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imehairishwa hadi Novemba 11 mwaka huu baada ya mshtakiwa kudai afya yake haiko sawa.

Mtuhumiwa huyo anayeshtakiwa kwa makosa 64 ikiwemo  kuendesha gari kwa uzembe katika barabara ya umma Mwanza- Shinyanga na  kusababisha vifo, majeruhi pamoja na uharibifu wa mali amepandishwa kizimbani leo Novemba 5, 2024 kwa mara ya pili mbele ya Ester Maliki Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi.

Baada ya kupandishwa kizimbani mtuhumiwa huyo aliomba kuahirishwa kwa kesi  hiyo na kupangiwa tarehe nyingine kwa kunyanyua mkono na kuruhusiwa kuzungumza kabla ya kuanza kusomewa hoja za awali na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Lilian Meli ambapo baadae hakimu Ester Maliki aliridhia ombi hilo.

“Kwa kuwa mshtakiwa ameomba kuwa hali yake kiafya siyo nzuri basi tunaahirisha shauri hili hadi tarehe 11 mwezi wa 11 mwaka 2024,” amesema Hakimu Ester.

Dereva wa basi la Asante rabi Shedrack Swayi (37) akiingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Misungwi.Picha| Mariam John/Nukta.

Kwa sasa mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya wadhamini wake kutimiza masharti ya dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks