KAN Festival: Tamasha linalolenga kuchochea maendeleo Afrika
Tamasha hilo linalenga kudumisha tamaduni za Kiafrika ili kuchochea maendeleo. Picha | KAN Festival
- Ni tamasha la tatu kufanyika linalolenga kudumisha tamaduni za Afrika.
- Lilianza kufanya Januari 1 mwaka huu na kilele chake ni Januari 28, 2020 jijini Arusha.
- Linawakutanisha pamoja wadau wa maendeleo, sanaa, utamaduni, habari na teknolojia.
Dar es Salaam. Huenda tamaduni za Afrika zikaimarika zaidi siku zijazo, baada ya wadau mbalimbali wakiwemo wasanii kukutana pamoja katika tamasha la maarifa ili kujadili namna fikra mpya zinavyoweza kuleta maendeleo barani humo.
Tamasha hilo la maarifa na sanaa (KAN Festival) ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa linalenga kudumisha tamaduni za Kiafrika ili kuchochea maendeleo ya fikra na matendo yanayoweza kuleta mabadiliko chanya katika nchi mbalimbali za Afrika.
Tamasha hilo lililoandaliwa na Kituo Cha Mafunzo na Maendeleo (MS TCDC) kwa kushirikiana na washirika kutoka Afrika Mashariki na wadau katika tasnia ya sanaa, habari na teknolojia lilianza tangu Januari 1, 2020 na kilele chake kitakua Januari 28, 2020.
Tamasha hilo linafanyika kwa njia ya mtandaoni na wadau kukutana Usa River jijini Arusha. kujadili mstakabali wa Afrika na tamaduni zake katika kuleta maendeleo endelevu.
Baadhi ya shughuli zinazofanyika katika tamasha hilo ni pamoja na semina, warsha, majadiliano na maonyesho ya bidhaa za sanaa na utamaduni ambazo zinasadifu maendeleo ya bara la Afrika.
Licha ya changamoto mbalimbali na majanga asilia kutokea ikiwemo Corona, umuhimu wa tamasha hilo linasaidia kutathmini maendeleo na na mbinu bora zitakazoendesha mabadiliko ya kimfumo katika bara la Afrika.
Zinazohusiana:
- TAMASHA LA NISHATI LA WANAHABARI 2018: Wadau wataka changamoto za nishati jadidifu ziangaliwe upya
- Tamasha la ‘Urithi Festival’ kufanyika mikoani kila mwaka
Mkurugenzi wa KAN Festaival, Khalila Mbowe amesema hata baada changamoto zilizotokea karibuni jambo la muhimu ni kuhakikisha watu wanasonga mbele kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
“Katika kipindi ambapo Afika na dunia inapitia changamoto mbalimbali tamasha letu liinatoa mwanga kwa kwa ajili ya maendeleo yetu kwa pamoja,” amesema Mbowe.
Aidha, amesema tamasha hilo limeandaliwa maalum kwa ajili ya vijana, wanaharakati, wasanii, watunga sera hata sekta binafsi ili kuhakikisha lengo la kuijenga Afrika linafikiwa kwani makundi hayo yana uwezo mkubwa na ni nguvukazi iliyo imara.
Tamasha la mwaka huu ni mwendelezo wa tamasha la mwaka jana ambalo liliangazia namna maendeleo ya watu kwa kauli mbiu ya “Maendelo ni watu, siyo vitu,”