Kama ni mahaba basi filamu ya “The Photograph” ni mwisho wa reli

March 20, 2020 8:25 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Ni zaidi ya mahaba shata shata. Picha| Ap News.


  • Ni filamu inayosimulia kisa cha mpigapicha na mwanaye
  • Itakufundisha dhana nzima ya mapenzi na changamoto zake.
  • Imesheheni waigizaji wenye nyota zao kwenye tasnia ya uigizaji.

Dar es Salaam. Baadhi ya watu wanafanya kazi wakiwa nyumbani, wengine wakiendelea kwenda maofisini na wengine wakiwaza ni nini watafanya wikiendi hii inavyoanza hasa baada ya mikusanyiko ya watu wengi kuzuiliwa na Serikali ikiwemo michezo.

Kama bado unawaza ni nini utafanya wikiendi hii, www.nukta.co.tz inakusogeza karibu na burudani ya filamu ambayo unaweza kuifanya kama burudani yako kwenye huu mwisho wa wiki.

Huenda ni siku nyingi tangu siku ya wapendanao iishe lakini mapenzi hayategemei siku hiyo kwani filamu ya The Photograph inayoonyeshwa katika kumbi za sinema itakufanya “Ufall in love” tena na tena.

Filamu hii inaongelea maisha ya mpiga picha Christina Eames (Chanté Adams) anayefariki ghafla na kumuacha mwanae Mae Morton (Issa Rae) akiwa na maswali mengi, hasira na njiapanda kubwa maishani mwake.

Pale hifadhi ya picha za mama yake inapopatikana, Mae anaanza safari ya kujitafuta huku akijikuta akidondoka kwenye penzi la mwandishi wa habari nyota ambaye alifuatilia maisha ya mama yake kabla ya kifo chake.

Mahaba shata shata, penzi zito kiasi cha mwana mieleka Joncena kushindwa kulibeba linasimuliwa kwa visa visivyoshikika.


Zinazohusiana


Tazama filamu hii kwenye ukumbi za Mlimani City pekee kwa Sh10,000. Habari njema ni kwamba, Kampuni ya Century Cinemax ambayo inamiliki kumbi hiyo imesema haitojaza watu bali kutakuwa na nafasi ya kutosha baina ya mtu na mtu ili kuepusha maambukizi ya Corona.

Bila kusahau vitakasa mikono, usafi wa vitasa kila kishikwapo na mtu utazingatiwa.

Unaachaje kujionea filamu hii iliyoandikwa na kuongozwa na Stella Meghie iliyogharimu kiasi cha Sh36.99 bilioni? Jifunze jinsi mapenzi yanavyochukua nafasi na kubadilisha maisha yetu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV