Jinsi ya kuzungumza na mtu kuhusu chanjo ya Uviko-19

August 27, 2021 8:11 am · Medlini
Share
Tweet
Copy Link
  • Wape watu fursa kutoa maoni yao kuhusu chanjo.
  • Wape taaarifa za sahihi kuhusu chanjo na faida zake.

Dar es Salaam. Ni dhahiri kuwa chanjo ya Uviko-19 imepokewa kwa namna tofauti kwenye jamii. Wapo ambao tayari wamechanja lakini wengine hawana mpango kabisa.Wengine wanasubiri watu wengi wachanje ndipo na wao waungane nao. 

Ili watu wajitokeze kuchanja, wanatakiwa kuelimishwa kuhusu umuhimu wa chanjo kwa sababu inagusa moja kwa moja afya zao.

Zipo mbinu mbalimbali za kuzungumza na mtu kuhusu chanjo hasa wasiotaka na wale ambao bado wanasita kufanya maamuzi. 

Shirika la afya Duniani (WHO) limetoa mwongozo ambao umeweka wazi njia nne za kuzungumza na mtu kuhusu chanjo ya Uviko-19:

Sikiliza kwa makini

Mpe nafasi ya kuzungumza mtu mwenye wasiwasi kuhusu chanjo. Msikilize hoja zake bila kumpinga, kisha mueleza kwa kina kuhusu chanjo na faida zake. 

Hakikisha unajibu maswali yake kwa ufasaha na kumuondolewa kila shaka aliyonayo ili kumfanya akubali kuchanjwa.

Uliza maswali

Pia kuuliza maswali ya wazi  kama vile “Umesikia nini juu ya chanjo za Uviko-19?”, maswali haya husababisha majibu zaidi ya “ndiyo” au “hapana” na yanaweza kukusaidia kuelewa vizuri shida za watu wanaotakiwa kupata chanjo. Pia inaweza kumsaidia mtu mwingine kufanya kazi kupitia mawazo yao.

Toa taarifa sahihi

Mpatie mtu taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu chanjo ambazo zinatoka katika mamlaka za afya ikiwemo WHO. Kabla ya kuzungumza na mtu omba idhini yake ili kuepuka kuonekana unamshinikiza kuhusu kupata chanjo.

Kama huna majibu ya uhakika kuhusu swali uliloulizwa, usijibu badala yake tafuta taarifa za uhakika kuhusu jambo husika.

Eleza faida za kupata chanjo

Wakati wa kujadili kuhusu chanjo, pia toa sababu zako za kutaka kupata chanjo na ikiwa uko katika nafasi nzuri eleza uzoefu wako jinsi itakavyosaidia kukinga familia na jamii na kurudisha shughuli na raha za maisha ambazo zilikuwepo kabla ya uwepo wa Uviko-19.

Hata hivyo, mashirika mbalimbali ndani na nje ya sekta ya afya yanaweza kuchukua jukumu muhimu katika kutoa habari sahihi juu ya  chanjo na faida zake.

Hiyo inaweza kusaidia watu kujitokeza na kupata chanjo kwa wingi.

Pia  mashirika hayo yanatakiwa kuongoza kwa mfano yaani kusaidia katika utoaji wa chanjo, kujenga uaminifu yaani kusikiliza maswali na kutoa ushauri kuhusu chanjo na pia kusaidia katika kuvunja vizuizi vya aina yoyote juu ya chanjo.

Ikiwa watu wataelekezwa kwa ufasaha, uwezekano wa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ni mkubwa.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW