Jinsi ya kuhamisha “chati” za WhatsApp kutoka simu za Android kwenda iPhone
- Whatsapp inatarajia kuachilia huduma hiyo hivi karibuni.
- Itarahisisha watumiaji wa Android kubaki na chat zao hata wanapohamia IOS.
- Mfumo huo utaambatana na sasisho la WhatsApp kwenye IOS la hivi karibuni.
Dar es Salaam. Kila mara unaposasisha simu kutoka kutumia simu za android kwenda simu za IOS, ni kama unaanza maisha upya. Mbali na kupoteza baadhi ya kumbukumbu kama picha na taarifa za apps, unaweza kupoteza mazungumzo yako na uwapendao.
Utapoteza kumbukumbu zako ikiwemo chati ambazo ulikuwa nazo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kama WhatsApp na meseji za kawaida. Kwa mitandao mingine kama Instagram na Telegram, walau una uhakika wa kukuta chati zako popote utakapohamia.
Hata hivyo, henda siku za usoni, hiyo isiwe changamoto tena kwani tayari wabunifu wapo kazini. Wabunifu kutoka mtandao wa WhatsApp wapo mbioni kuzindua mfumo ambao utawawezesha watumiaji wa simu za Android kuhama na “chat” zao pale wanapobadilisha simu na kuanza kutumia simu zenye mfumo endeshi wa iOS ambazo ni iPhone.
Tovuti ya masuala ya kiteknolojia, Andorid Central imesema mabadiliko hayo tayari yanaonekana kwenye app ya WhatsApp Messenger beta for iOS ambayo ni app ya majaribio inayotarajiwa kusasisha toleo linalotumika sasa.
Android Central imeeleza kuwa, mwaka jana WhatsApp ilikuwa ikizungumza na Apple pamoja na Google ili kuruhusu watumiaji wa simu zao kuweza kuhama na chati zao pale wanapobadilisha simu.
Mfumo huo unafanya kazi kwenye simu zote yaani kutoka Android kwenda IOS na IOS kwenda Android.
Soma zaidi:
- Mbinu tano za kubaini habari feki WhatsApp
- Jinsi ya kuhamisha mawasiliano WhatsApp kwenda Telegram
- Uunganishwaji wa WhatsApp, Facebook na Instagram bado sana
Kati ya vitu vya kuzingatia ni pamoja na kuhakikisha kuwa simu zote yaani inayohamisha na inayohamishiwa zina chaji walau asilimia 80.
Pia ni muhimu kufahamu kuwa, endapo utaruka (skip) hatua ya kuhamisha chati hizo, hautoweza kufanya tena jambo hilo.
Mfumo huu utaanza kufanya kazi pale WhatsApp itakapoingiza sasisho hilo kwenye maduka ya programu za Apple ya App Store.
Ili kujua hatua kwa hatua ya jinsi ya kuhamisha chati kutoka simu ya Android kwenda IOS, endelea kusoma www.nukta.co.tz.
Latest
