Je unakumbuka njia za kujikinga na Uviko-19?

September 1, 2022 12:32 pm · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Nenda kapate chanjo ya ugonjwa huo.
  • Nawa mikono, vaa barakoa na epuka mikusanyiko ya watu wengi.

Dar es salaam. Ni takribani miaka mitatu sasa tangu ugonjwa wa Corona (Uviko-19) uikumbe dunia na kusababisha watu kuugua na wengine hata kufa.

Katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi, Agosti 25 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk. Tedros Ghebreyesus alitoa wito kwamba watu hawapaswi kujisahau wala kuchukulia kama janga la Uviko-19 limeisha kwa sababu linaendelea kuua mamilioni ya watu duniani.

Hata hivyo serikalii duniani zimeendelea na juhudi mbalimbali za kupambana na janga hilo ikiwemo utoaji chanjo kwa  watu wa rika mbalimbali.

Jitihada hizi za kukabiliana na Uviko-19 hazipaswi kufanywa na serikali tu lakini watu pia kushirikishwa kukabiliana na janga hili la ulimwengu.


Soma zaidi


Mambo muhimu ya kuzingatia kujikinga na Corona

1. Kumbuka kunawa mikono kila mara kwa kutumia sabuni na maji tiririka kwa angalau sekunde 20, ama tumia kitakasa mikono. Kwa kufanya hivyo utakuwa unajikinga na Uviko-19.

2. Kumbuka kuvaa barakoa unapokua sehemu zenye watu wengi kama vile sokoni ama kwenye usafiri wa umma. Hii ni muhimu hasa katika maeneo yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huo.

3. Epuka kushika macho, pua, ama mdomo wako. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kusambaza virusi kwenye maeneo hayo ambayo ndio njia kuu ya kupitisha virusi hivyo.

4. Funika mdomo wako na pua kwa kutumia kiwiko ama tishu unapokohoa ama kupiga chafya. Tupa tishu sehemu salama baada ya kuitumia.

5. Kumbuka kukaa umbali kati yako na watu wengine kadiri inavyowezekana. Hii inamaanisha kukaa umbali wa mita 2 kati yako na watu wengine, haswa wale wenye dalili za kuumwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV