Jambazi sugu ndani ya mwili wa binti asiye na hatia

November 13, 2020 8:50 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inamhusu binti mpole na asiye na mvuto kwa marafiki wawili na siyo watu wengine.
  • Binti huyo anakuwa “target” ya jambazi sugu anayetafutwa na polisi kila kona.
  • Kwa kutumia nguvu za ajabu, jambazi huyo anafanikiwa kuiba mwili wa binti Kessler na kumwacha binti huyo ndani ya mwili wake.

Dar es Salaam. Ni ijumaa nyingine iliyo tofauti na zingine ambayo tunakuletea uchambuzi wa filamu yenye maudhui ya kufikirika ya “Freaky” ambayo itasaidia kukamilisha wikiendi yako.

Millie Kessler ni mwanafunzi wa sekondari na kutokana na mavazi yake na jinsi anavyojiweka, hana mafanikio ya kutiliwa maanani na mtu yeyote shuleni hapo isipokuwa rafiki zake.

Kwa watu, binti Kessler ndiyo ngoma ya kijiji kwa maana ya kwa kila anayejisikia kuonea mtu, mtu wa kwanza kumfikiria ni binti huyo ambaye kwa shule nzima, amefanikiwa kuwa na marafiki wawili tu.

Sifa za binti huyo, zinafanikiwa kukonga moyo wa muuaji matata maarufu kama Butcher ama Barney Garris. Kwa kutumia nguvu za ajabu, Butcher anamuwinda Kessler na kufanikiwa kubadilishana naye mwili.

Sura ya kipole, kudharauliwa na watu na kutotiliwa maanani ni mwili ambao muuaji yeyote angependa kuutumia.

Butcher aanza harakati zake

Butcher ambaye sasa yupo ndani ya mwili wa Kessler, anaanza kutekeleza mauaji yake kwa wanafunzi wa shuleni kwa Kessler! Ndiyo! Najua umeelewa.

Kwa upande mwingine, Kessler ambaye sasa yupo ndani ya mwili wa mwanaume anapitia wakati mgumu kwani hata rafiki zake wanamkimbia kwa hofu ya kuuliwa hadi pale anapowadhihirishia kuwa, ni yeye ila tu akiwa ndani ya mwili ambao siyo wake.


Soma zaidi:


Hata hivyo, bahati mbayani kuwa, akiwa ndani ya mwili wa muuaji huyo, anaanza kutafutwa na vyombo vya dola ili atiwe nguvuni na kuhukumiwa kwa mamia ya mauaji aliyoyafanya.

Kessler ana muda wa chini ya saa sita kufanya kila awezalo ili arudi kwenye mwili wake au la sivyo, atabaki ndani ya mwili wa Butcher milele?

Fuatilia kisa cha filamu hii kupitia kumbi za kuangalizia filamu za Century Cinemax zilizopo katika maduka makubwa jijini Dar es Salaam yakiwemo Mlimani City na Aura Mall.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV