Jafo: Takwimu za hali hewa zitumike katika tathmini za mazingira

February 19, 2022 6:15 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Aagiza miradi inayoanzishwa kutumia takwimu za hali ya hewa.
  • Hayo ni matakwa ya Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ya 2019.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amewaagiza wadau wa mazingira kutumia takwimu sahihi za hali ya hewa katika kuandaa tathmini za athari kwa mazingira nchini.

Amesema hatua hiyo ni kutekeleza matakwa ya sheria namba 2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. 

Jafo ametoa maelekezo hayo wakati akifungua rasmi warsha ya wadau wa mazingira kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa, iliyofanyika katika Ukumbi wa Maktaba, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jana Februari 18, 2022.

“Nikiwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) nitahakikisha kabla ya kutoa vyeti tathmini za athari kwa mazingira (EIA), jambo kubwa nitakaloliangalia ni chanzo cha takwimu zilizoambatanishwa, hivyo hakuna namna ya kukwepa, tutumie takwimu sahihi za hali ya hewa kwa mustakabali wa nchi yetu,” amesema Jafo.

Amesema kila mradi unaotaka kuwekezwa unatakiwa kufanyiwa tathmini za athari za mazingira, na mchakato wa EIA ni lazima unahitaji takwimu za hali ya hewa, na ikitokea umekosea takwimu utaleta shida.

Aidha, Jafo ameeleza kuwa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaipa mamlaka hiyo jukumu la kutoa takwimu za hali ya hewa na kuzitaka wizara, taasisi na wataalam elekezi wa mazingira kuzingatia umuhimu wa matumizi ya takwimu za hali ya hewa na endapo takwimu hizo zitakosekana inatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka TMA na kutokufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.


Soma zaidi: 


Vilevile, Jafo ameitaka TMA kuandaa semina kwa maafisa mazingira waliopo katika halmashauri na mikoa yote nchini ili wafahamu vyema masuala muhimu ya hali ya hewa kama ilivyoainishwa katika sheria. 

Pia kutoa mada kwenye vikao vya wakurugenzi wa jiji na halmashauri, ili kuwajengea uelewa wa sheria hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi amesema kuwa warsha hiyo ni fursa  muhimu ya kuboresha huduma katika sekta ya mazingira kwa kuzingatia matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa zinazotolewa na TMA na matakwa ya kisheria pamoja na kuimarisha uelewa kuhusiana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.

Aidha, Dk Kijazi ambaye ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) amewajulisha washiriki wa warsha hiyo kuwa huduma za hali ya hewa zinazotolewa nchini zimeongezeka viwango vya usahihi hivyo zinafaa kutumika katika sekta zote za maendeleo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
9 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
9 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Nukta TV

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV