INEC yasisitiza Mpina, Ferej si wagombea Urais Tanzania

September 22, 2025 3:39 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • ACT Wazalendo yaaswa kuzingatia sheria za  uchaguzi.

Arusha. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesisitiza uamuzi wake kuwa Luhaga Mpina na Fatma Ferej hawajapitishwa na tume hiyo kugombea nafasi ya Urais nchini Tanzania.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima, iliyotolewa leo Septemba 22, 2025 imesema kuwa imebaini Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kuwatambua wagombea hao katika matukio ya chama hicho kama wagombea Urais taarifa ambayo si sahihi.

“Tunasisitiza kwamba, chama cha ACT Wazalendo hakina wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025..

…Kwa kuzingatia uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wa tarehe 15 Septemba, 2025 uliotengua uteuzi wa Ndugu Luhaga Joelson Mpina aliyependekezwa na chama hicho kugombea Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,’ imesema taarifa ya Kailima.

Msisitizo huo wa INEC unakuja ikiwa zimesalia siku 37 kufikia Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani huku ACT Wazalendo ikiendelea kuweka mapingamizi mahakamani juu ya uamuzi wa kufutwa kwa mgombea Urais kupitia chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa ya ACT Wazalendo iliyotolewa jana Septemba 21, 2025 pingamizi hilo la INEC la khA kumuondoa Mpina katika orodha ya wagombea uchaguzi litasikilizwa leo katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma mbele ya Majaji watatu ambao ni Jaji Sylvester Kainda,  Jaji Fredrick Manyanda, na Jaji Abdallah Gonzi.

ACT Wazalendo bado inaendelea kumtambua Luaga Mpina (pichani) kama mgombea Urais kupitia chama hicho.Picha/ACT Wazalendo/Instagram.

Aidha, INEC imeitaka ACT Wazalendo kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ikiwemo kuheshimu ratiba ya uzinduzi wa kampeni za ubunge katika maeneo husika

“Tunashauri na kusisitiza kuwa, Chama cha ACT Wazalendo kizingatie masharti ya Kanuni ya 35 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 inayohusu utaratibu na ratiba za kampeni za ubunge,” imesema taarifa ya Kailima.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV