INEC yamuondoa tena Mpina kwenye kinyang’anyiro cha Urais Tanzania

September 15, 2025 11:51 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kushinda kesi ya dhidi ya INEC siku nne zilizopita

Arusha. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemuondoa tena  Luhaga Mpina kwenye kinyanganyiro cha urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Uamuzi huo wa INEC unakuja ikiwa ni siku nne tangu Mpina ashinde kesi dhidi ya tume hiyo kuhusu shauri la maombi ya Kikatiba akipinga kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 na siku mbili tangu INEC imteue kuwa mgombea Urais.

Taarifa ya  Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhani Kailima, iliyotolewa leo Septemba 15, 2025 inabainisha kuwa uamuzi huo umetokana na pingamizi lililowasilishwa na Hamza Saidi Johari, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Hivyo, jina la Ndugu Luhaga Joelson Mpina, mgombea wa kiti cha Raiskupitia Chama cha ACT-Wazalendo limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025,” imesema Taarifa ya Kailima.

Aidha, INEC imetupilia mbali pingamizi la Mpina dhidi ya Samia Suluhu  mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kesi nyingine mbili.

Mapingamizi hayo ni pamoja na  lililowekwa na Almas Hassan Kisabya mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chama cha NRA dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo

Pingamizi lingine ni lile lililowekwa na Kunje Ngomale Mwiru mgombea kiti cha Rais kupitia chama cha AAFP dhidi ya Ndugu Luhaga Joelson Mpina mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
20 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
20 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MNAOSEMA Magufuli mbali hii inawahusu! Meneja atia neno

MNAOSEMA Magufuli mbali hii inawahusu! Meneja atia neno

Nukta TV

Hakuna mwenye kibali cha kupakia abiria nje ya Stendi ya Magufuli

Hakuna mwenye kibali cha kupakia abiria nje ya Stendi ya Magufuli

Nukta TV

Hali ilivyo Stendi ya Magufuli, utaratibu wa kupakia abiria upo hivi!

Hali ilivyo Stendi ya Magufuli, utaratibu wa kupakia abiria upo hivi!

Nukta TV