IGP Wambura apangua makamanda wa Polisi

June 17, 2025 12:56 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayofanyika ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwahamisha makamanda watatu wa polisi katika mikoa na vitengo mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya kawaida ndani ya jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iloiyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime leo Juni 17, 2025 imeeleza kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID) yaliyopo jijini Dodoma.

Awali Katabazi alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma  na nafasi ya yake sasa itashikiliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Galus Hyera, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli kabla ya uhamisho huo.

Katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matride Kuyeto, aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, amehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli.

Jeshi la Polisi halijatoa sababu maalum za uhamisho huo, lakini limeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida na hufanyika kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ndani ya taasisi hiyo ya usalama.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV