Hizi ndio nchi 5 zenye idadi kubwa ya Simba Afrika

December 5, 2025 12:35 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Tanzania yashika kinara, yarekodi simba 14,500.
  • Ni pamoja na Zambia, Kenya na Afrika Kusini.

Arusha. Sekta ya utalii ni kati ya sekta muhimu zinazotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Pamoja na uwepo wa vivutio lukuki vya utalii vinavyotokana na vyanzo mbalimbali, wanyama pia akiwemo simba wamekuwa wakivutia mamilioni ya watu kutoka maeneo mbalimbali duniani kufanya utalii.

Simba, ambao mara nyingi huitwa ‘wafalme wa nyika’ huvutia zaidi kutokana na uzuri, nguvu pamoja na maisha anayoishi nyikani wakisaidia kusawazisha mfumo wa ikolojia.

Licha ya uzuri wa wanyama hao, Shirika la Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi na Kulinda Uasilia (IUCN) linawataja simba kuwa miongoni mwa viumbe walio hatarini kupotea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujangili na kuharibika kwa makazi yao. 

Utalii ni miongi mwa shughuli ya kiuchumi inayoingizia fedha mataifa mbalimbali Afrika na duniani. Picha/ Serengeti.

5. Zambia

Zambia ni nchi iliyopo kusini mwa Afrika, ikijulikana zaidi kwa uwepo wa maporomoko ya ziwa Victoria na wanyamapori mbalimbali. Uchumi wa nchi hiyo unategemea zaidi shaba na sekta ya utalii inayokua kwa kasi.

Shirika la World Population Review inaitaja Zambia kuwa na jumla ya simba 2,346 waliopo katika mbuga na hifadhi mbalimbali zilizopo nchini humo.

4. Kenya

Kenya inayosifika kwa sekta imara ya utalii ina jumla ya Simba 2,515 ambao wapo katika hifadhi mbalimbali nchini humo ikiwemo Maasai Mara, Amboseli na Tsavo.

Katika hifadhi hizo unaweza kujionea wanyama wengine (wakubwa Big Five) mbali na simba akiwemo tembo, twiga, chui, na faru.

Ukiwa nchini humo unaweza kufanya shughhuli nyingine za utalii ikiwemo Safari za magari (Game drives), kutazama na kupiga picha na ndege pamoja na utalii wa angani kupitia ‘Hot Balloon Air Safaris’.

Simba dume wakimla nyati katika mbuga ya wanyama ya Tsavo nchini Kenya. Picha/ Tsavo.

3. Botswana

Botswana inayojulikana zaidi kwa uwepo wa Delta ya Okavango na Jangwa la Kalahari ina idadi ya simba 3,063 kutoka mbuga mbalimbali zilizopo nchini humo.

Licha ya sekta ya utalii humo kuendelea kukua taratibu, SafariBookings.com imeitambua Botswana kuwa nchi bora ya safari Afrika (Africa’s Best Safari Country) kwa mwaka 2025,

Miongoni mwa hifadhi maarufu nchini Botswana ni Okavango Delta, Hifadhi ya Taifa ya Chobe, Moremi, Makgadikgadi Pans, na Nxai Pan.

2. Afrika Kusini

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi maarufu barabi Afrika ikisifika kwa Mandhari ya kuvutia itokanayo na fukwe, safu za milima, savanna, na shamba kubwa la mizabibu linalojulikana kama Cape Winelands.

Pamoja na umaarufu huo, Afrika Kusini inasifika pia kwa shughuli za utalii zinazochochewa na uwepo wa aina nyingi za wanyama ikiwemo simba ambao shirika la linabainisha kuwa wapo  3,284.

Mbali na wanyama Tanzania pia inasifika kwa vivutia vizuri ikiwemo mlima Kilimanjaro uliopo mkoani Kilimanjaro. Picha Safar Booking.

  1. Tanzania

    Shirika la World Population Review limeitaja Tanzania kuwa na simba 14,500 idadi inayoifanya kuwa kinara wa idadi kubwa ya Simba barani Afrika.

    Katika mbuga zake za kitaifa na mapori ya akiba nchini Tanzania, unaweza kuona simba jike wakiwinda alfajiri, madume wakinguruma na wengine wakiwinda au kupumzika katika vivuli vya miti.

    Unaweza kujionea wanyama hao katika hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti, Ngorongoro, Tarangire na Ruaha.

    Hata hivyo, takwimu hizo zinatofautiana na zile zilizotolewa na IUCN pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ambao waliripoti idadi ya simba hao kuwa 17,000.

    Pamoja na hayo, Tawiri ilibainisha kuwa Tanzania imeongoza barani Afrika kwa kubwa na idadi kubwa ya wanyama wengine ikiwemo Nyati na Chui.

    Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *

    Follow Us on TikTok

    Subscribe to Our YouTube Channel

    Subscribe

    Loading videos...

    Loading videos...

    Loading videos...

    Enable Notifications OK No thanks