Hajatulia: Rais Samia amteua Maharage Chande kuwa Postamasta Mkuu

September 26, 2023 4:31 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni siku mbili tangu alipomteua kuwa Mkurugenzi wa TTCL.
  • Avunja bodi ya Rea, ateua Mkurugenzi mpya.

Dar es Salaam. Unaweza kusema kuwa Maharage Chande aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco) alikuwa safarini kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa bosi wa Shirika la Posta akimhamisha kutoka nafasi yake mpya aliyehudumu kwa siku mbili tu. 

Chande ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu wa Posta ikiwa zimepita siku mbili tu tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) akitokea Tanesco alikohudumu kwa kipindi cha miaka miwili tangu Septemba 2021.

Katika uteuzi huo uliotangazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, Chande anachukua nafasi ya Macrice Mbodo ambaye atapangiwa majukumu mengine. 

Kutokana na uteuzi huo mpya, Yunus ameeleza kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL kabla ya Chande, Peter Ulanga ataendelea na majukumu yake ya awali.


Soma zaidi : Rais Samia apangua vigogo TTCL, Tanesco, vilio vya umeme vikiendelea Tanzania


Chande anaingia kwenye orodha ya watendaji wakuu wa taasisi za umma waliohudumu kwa muda mfupi katika nafasi zao akiwemo Thobias Mwesiga Richard aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) April 4, 2021 na kisha kufutwa kazi siku moja baadaye. 

Mapema leo, Chande alikuwa kwenye mkutano na Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari ya Mawasiliano, Nape Nnauye aliyemtania Chande kuwa mshale umerudi nyumbani. 

Hata hivyo, mabadiliko ya leo yataendelea kumfanya Chande kuwa chini ya wizara hiyo ya Nape. 

Siku za hivi karibuni kumekuwa na panga pangua mfululizo, zinazofanywa na Rais Samia kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma, ambapo baadhi ya vigogo wamehamishwa katika nafasi zao na wengine kuahidiwa majukumu mengine.

Kuhamishwa kwa Chande kutoka Tanesco katika kipindi ambacho nchi inakabiliwa na mgao wa umeme kutokana na upungufu wa nishati hiyo ni miongoni mwa mambo yaliyozua mjadala mtandaoni siku mbili hizi.

/span>

Pia, mabadiliko ambayo bado yapo midomoni mwa watu ni uteuzi wa aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Said Othman Yakubu ambaye ameteuliwa kuwa balozi. 

Hadi sasa kumekuwa na mjadala wa mtu atakeyerithi kiti chake kuwa baadhi ya watumiaji wa mitandao wakitaja taja majina ya wanahabari nguli nchini kuwa huenda mmoja wao akatoboa.


Soma zaidi : BOT kununua dhahabu kwa wafanyabiashara, wachimbaji wa ndani


Bodi ya Rea yavunjwa

Aidha taarifa ya Ikulu imebainisha kuwa Rais Samia amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA)  ambapo  amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Rea.

Katika uteuzi wa leo, Rais Samia pia ameteua Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) John Ulanga kuwa balozi.

‘Uteuzi huu unaanza mara moja na Balozi Mteule Bw. Ulanga ataapishwa tarehe 26 Septemba, 2023 Ikulu, Dar es Salaam,” inabainisha taarifa hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV