Guterres: Hakuna jamii itakayokuwa huru na haki bila waandishi wa habari

October 9, 2021 7:02 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Vyombo vya habari ndiyo msingi wa demokrasia ya kweli.
  • Ataka vyombo vya habari viheshimiwe na kulindwa.
  • Wapongeza wanahabari wawili waliopata tuzo ya Nobel mwaka 2021.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amewapongeza waandishi wa habari Maria Ressa na Demirty Muratov kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu akisema uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu katika ujenzi wa demokrasia duniani.

Maria, mwandishi wa habari za uchunguzi wa Ufilipino na mwandishi wa habari wa Urusi, Muratov wametunukiwa tuzo ya Nobel kwa mwaka 2021 kwa kuwa mstari wa mbele kulinda uhuru wa kujieleza duniani licha ya changamoto wanazokutanazo katika shughuli zao.

“Duniani kote uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ajili ya amani, haki, maendeleo endelevu na haki za binadamu na ni ngumo muhimu kwa ajili ya ujenzi wa taasisi zenye haki na zisizo na upendeleo,” amesema Guterres. 

Katika taarifa yake ya Oktoba 8, 2021 ya pongezi kwa washindi hao, Guterres amesisitiza kuwa “hakuna jamii inayoweza kuwa huru na haki bila waandishi wa habari ambao wanaweza kuchunguza maovu, kufikisha taarifa kwa umma, kuwawajibisha viongozi na kuzungumza ukweli kwa mamlaka.” 

Licha ya ukweli huo bado vyombo vya habari vinaendelea kupingwa na mashambulizi dhidi ya wanahabari yanaendelea kuongezeka duniani. 

“Tunashuhudia machafuko yakiongezeka na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari wa ana kwa ana au mtandaoni. Wanawake waandishi wa habari mara nyingi ndiyo walengwa wa ukatili huo,” amesema. 

Katibu Mkuu amesema wakati huo huo teknolojia imebadili njia za watu kupokea na kubadilishana taarifa , pia inatumika kupotosha maoni ya umma au kuchochea machafuko na chuki. 

“Uongo  wa kupinga ukweli, na hii haiwezi kuwa kawaida mpya. Uandishi wa habari huru na wa kujitegemea ni mshirika wetu mkubwa katika kupambana na habari potofu na upotoshaji,” amesisitiza Guterres.

Amezitaka serikali duniani kutambua jukumu la msingi la waandishi wa habari na kuelimarisha juhudi katika kila ngazi kusaidia vyombo vya habari huru vya kujitegemea na vya aina mbalimbali. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

CEO, TAB Group: Africa Agri Expo 2026 inakwenda kufungua fursa kimataifa, kilimo cha Tanzania

Nukta TV