Google kuipa sura mpya tasnia ya muziki duniani

January 31, 2023 11:53 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kupitia mfumo wa akili bandia uitwao MusicLM.
  • Programu hiyo inamuwezesha mtu kutengeneza muziki kwa maandishi. 
  • Programu hiyo ikitoka inatajwa kuleta mapinduzi ya muziki duniani. 

Dar es Salaam. Huenda kazi ya wasanii kuandaa muziki ikarahisishwa zaidi katika siku zijazo au pengine watu wasihitaji wanamuziki ili kuwaburudisha kwa sababu wataweza kutengeneza  wenyewe kwa urahisi kwa kutumia zana na programu za akili bandia (AI).

Watafiti wa kampuni ya Google wametengeneza mfumo wa akili bandia uitwao Music unaoweza kutengeneza vipande vya muziki kwa kuchakata vidokezo vya maandishi sambamba na kubadilisha ala za vyombo tofauti kama filimbi au ngoma kuwa ala nyingine za muziki.

Kwa mujibu wa chapisho la watafiti hao, programu ya MusicLM imeundwa kutokana na mfumo unaozalisha muziki wa hali ya juu kupitia mtandao wa intaneti. 

Programu hiyo  imefunzwa kwenye seti kubwa ya data ya muziki ya zaidi ya saa 280,000, na kuiwezesha kuzalisha kiotomatiki nyimbo za ubunifu za ala, aina na dhana mbalimbali kulingana na maelezo ya maandishi.

Zaidi ya hayo, MusicLM inaweza kuchukua maelezo kadhaa yaliyoandikwa kwa mfuatano (k.m. “wakati wa kutafakari,” “wakati wa kuamka,” “wakati wa kukimbia,” “wakati wa kutoa 100%) na kuunda aina ya “hadithi” ya sauti au simulizi ya dakika kadhaa. Hivyo inafaa kabisa kwa nyimbo wa sauti za filamu.

MusicLM pia inaweza kuelekezwa kupitia mchanganyiko wa picha na maelezo mafupi, au kutoa sauti inayozalishwa na aina mahususi ya chombo fulani. Sambamba na hayo, mfumo huo unaweza kuunda muziki unaotokana na asili ya maeneo, nyakati au mahitaji (k.m. muziki wa motisha kwa mazoezi).


Zinazohusiana:


Kulingana na watafiti MusicLM inaweza kutoa sauti ya hali ya juu kwa usahihi zaidi wa 24kHz kwa dakika kadhaa, pia mtumiaji anaweza kupiga wimbo ili kuifunza algoriti ya Akili Bandia kumpatia mapigo yanayofaa na anayotaka kusikia. 

Pia wamechapisha seti ya mafunzo ya Akili Bandia ya vipande 5,500 vya muziki ili kusaidia watafiti wengine wanaofanya kazi ya kutengeneza nyimbo kiotomatiki.

Ingawa haijaanza kutumika rasmi kwa sababu ya masuala ya hakimiliki, MusicLM ni ishara ya kile kinachokuja kwa kutumia AI kutengeneza muziki kutokana na maelezo ya maandishi.

“Tunakubali hatari ya uwezekano wa matumizi mabaya ya maudhui ya ubunifu yanayohusiana na kesi ya matumizi…Tunasisitiza kwa nguvu hitaji la kazi zaidi ya siku zijazo katika kukabiliana na hatari hizi zinazohusiana na kizazi cha muziki,” chapisho la waandishi wenza wa Google limeandika.

Licha ya Google, kampuni nyingine za teknolojia ikiwemo Meta, Microsoft, OpenAI na zinaendelea na jitihada za kufikia mipaka ya kila tasnia kwa kutumia teknolojia ya AI ili kutoa suluhu na kurahusisha maisha ya mwanadamu.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW