Filamu za “Escape Plan” na “Maleficent” kukiwasha kumbi za sinema wiki hii

October 18, 2019 1:23 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu mpya ambazo zimeingia sokoni na zitaonyeshwa kwa wiki nzima kuanzia leo.
  • Zimejaa visa vingi hasa kwa wapenzi wa filamu za ngumi na vita.
  • Zitaifanya wikiendi yako iwe ya mafanikio kuliko unavyofikiria.

Dar es Salaam. Unafahamu kama ukiwa na mapumziko mazuri wakati wa wikiendi, kuna uwezekano mkubwa hata kazi zako zikafanyika kwa weledi unaporejea kazini Jumatatu? 

Basi hii ndiyo sababu ya wewe kutupilia mbali “earphones” zako, kuachana na kompyuta yako na kutafuta kumbi za kuangalizia sinema zilizo karibu na wewe zikiwemo za Mlimani City, Aura Mall na Mkuki House za Jijini Dar es Salaam.

Katika kumbi hizo na nyingine, wiki hii kuanzia leo ijumaa ya Oktoba 18, 2019, utawaweza kutazama filamu mbili mpya ambazo zimeingia sokoni na kukupa burudani isiyo na kifani.

Ascape Plan

Baada ya kumuona Sylvester Stallone (Rambo) kwenye filamu ya “Rambo Last Blood”, sasa anaungana na kinara wa michezo wa mieleleka Dave Bautista,  Curtis Jackson (50 Cent) na mwanadada  Jaime King kukuletea filamu itakayomaliza “popcorn” zako kabla ya wakati.​

Filamu hiyo yenye dakika 87 iliyosimamiwa na muongoza filamu, John Herzfeld imegharimu takribani Sh74 bilioni ikiwa ni mwendelezo wa sehemu mbili zilizotoka awali yaani 2013 na 2018 ambazo zilishirikisha manguli wa filamu za kivita na ngumi akiwemo Arnold Schwarzenegger.

Ni mwendelezo wa sehemu mbili zilizotoka awali yaani 2013 na 2018 ambazo zilishirikisha manguli wa filamu za kivita na ngumi akiwemo Arnold Schwarzenegger. Picha| Mtandao.

Itakuwaje pale mwana dada  Jaime King ambaye ni mpenzi wa Stallone anatekwa?

Lipia Sh10,000 tu kuona jinsi Stallone, Bautista na 50 Cent wanavyominyana baada ya watu wa karibu kutekwa huku wapiganaji wao wakiungana kuwatetea dhidi ya maadui..

Maleficent: Mistress of evil

Hapo zamani za kale, upendo wa mtoto (Elle Fanning) asiye na hatia ulibadilisha moyo uliojaa uovu kuwahi kutokea. Hakika muda unabadilisha vitu vingi lakini haibadilishi kila kitu.

Pale Aurora (Elle Fanning) anapochumbiwa, mama yake mlezi Maleficent (Angelina Jolie) anapinga. Mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi pale mke mpya wa mfalme, anapojitangaza kuwa mama mpya wa Aurora.

Unaachaje kuangalia kisa hiki cha Jolie ambaye ni mwigizaji mkuu kwenye filamu ya  Tomb Rider, Mr & Mrs Smith. Picha|Mtandao.

Vita inaanza kati ya Maleficent na ufalme mpya inayochochewa na mke mpya wa mfalme Malkia Ingris (Michelle Pfeiffer).

Unaachaje kuangalia kisa hiki cha Jolie ambaye ni mwigizaji mkuu kwenye filamu ya  Tomb Rider, Mr & Mrs Smith na filamu zingine zaidi ya 45. Kutana na wahusika hao kujua mbivu na mbichi kwenye filamu hiyo.


Zinazohusiana


Kwa kuangalia filamu hizo, hautapumzisha akili yako tu bali unaweza kukutana na washikaji wa kitambo na marafiki wapya katika harakati za wikiendi yako.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW